| Damu ya mlinzi wa Kanisa ikitiririka baada ya kuumizwa na watu wasiojulikana. |
| Tabrenakulo ndogo ikiwa imeharibiwa na kulia ni Msalaba uliovunjwa. |
| Muuguzi mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Iringa Rustica Tung'ombe akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya mlinzi aliyeumizwa na kufukishwa hospitalini hapo leo. |
| Mlinzi aliyeumizwa na watu wasiojulikana akiwa amelazwa hospitalini. |
Kanisa Katoliki Parokia
ya Kihesa Jimbo la Iringa limevunjwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo
huku mlinzi wa Kanisa hilo Bathlomeo Nzigilwa akijeruhiwa nusura kuuawa.
Akitolea maelezo juu ya
tukio hilo kanisani hapo leo, mhuduma wa Kanisa hilo Sista Lucy Grace Mgata amesema
aligungua kuwa kunauvamizi umefanyika alfajiri alipofika kanisani hapo kwa
ajili ya kufungua milango ya Kanisa hilo ili kutayarisha vyombo vya Ibada ya
Misa ambazo hufanyika kila siku kuanzia saa 12:00 asubuhi.
“Nilifika hapa saa
11:40 alfajiri kwa ajili ya kufungua milango na kufanya maandalizi kwa ajili ya
Misa lakini nilipoukaribia mlango huo nikakuta mlinzi amekaa kwenye kiti huku
kichwa chake akikiwa kimeinamishwa chini na kufunikwa kofia nikajua amelala
lakini milango ikawa wazi. Nilopofika jirani nikaona damu inatiririka chini na
mwili wake ukiwa umelowa damu nikaenda kugonga nyumba ya padre kutoa taarifa
ndipo walipofika waamini mbalimbali tukasaidia” alisema.
Pamoja na kuvunjwa kwa milango
ya Kanisa hilo, ofisi ya parokia nayo imevunjwa huku vitabu, mafaili mbalimbali
na pamoj na kumbukumbu zikiwa zimechanwa na kuvurugwa ovyo kiasi cha
kutotamanika.
Mavazi ya ibada na
vifaa mbalimbali vya ibada vimeharibiwa vibaya, Taberenakulo ndogo nayo
ikiharibiwa, msalaba kuvunjwa pamoja na Hostia Takatifu zikimwagwa kila mahali.
Sista Mgata alisema
kuwa kuliwa na hela za watumishi wa artare walizokuwa wakichangishana kwa ajili
ya matumizi ya umoja wao pamoja na hela za chama cha kitume cha utume wa Fatima
zimechukuliwa japo bado hazijajulikana jumla yake japo kuwa funguo za teberenakulo
kubwa wanayohifadhia Ekaristi Takatifu hazijulikani zilipo.
“Kulikuwa na hela
ambazo watumishi wa artare walikuwa wakichangishana kwa ajili ya matumizi ya
umoja wao pamoja na fedha za chama cha kitume cha utume wa Fatima zimechukuliwa
ingawa sijajuwa jumla yake mpaka wao wenyewe waje waeleze kulikuwa na kiasi
gani pamoja na funguo za taberenakulo kubwa hazionekani” alisema sista Mgata.
Kwa upande wake
Katekista Agustino Luhama mhudumu wa ofisi ya Parokia amesema hela
anazozikumbuka kwa harakaharaka ambazo zimechukuliwa na wavamizi hao ni zaidi
ya shilingi laki tano.
“Hela ninazozikumbuka
kwa harakaharaka ambazo zimechukuliwa ni zaidi ya shilingi laki tano lakini
zingine sijapata idadi kwa sababu nilikuwa sijazijumlisha na zingine nilizipokea
jana kutoka kwa waamini mbalimbali” alisema Kat. Luhama.
Padre Aloyce Mdemu
ambaye pia ni Makamu wa Askofu wa jimbo hilo amesema bado ni mapema kujua
thamani ya uharibifu uliofanyika kwa kuwa bado wanaendelea na uchunguzi wa
vifaa vingine na maeneo mengine ambayo huenda hayajagundulika.
“Ni kweli tukio hili
limetokea na limetushtua sana hata kuumizwa nuzura kuuawa mlinzi wetu lakini
bado ni mapema sana kujua thamani ya uharibifu wa vitu vyote vilivyoharibiwa
kwa sababu tunaendelea na uchunguzi wa vitu vingine na maeneo mengine ambayo
huenda nayo yameharibiwa na hayajajulikana. Tutakapokuwa tumekamilisha, taarifa
zitatolewa” alisema Pd. Mdemu.
Muuguzi mfawidhi wa
hospitali ya Mkoa wa Iringa Rustica Tung’ombe amethibitisha kupokea majeruhi
huyo na kusema kuwa hali yake ni mbaya na japo kuwa anaendelea kupata matibabu.
“Ni kweli tumempokea
majeruhi Bathlomeo Nzigilwa mlinzi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Kihesa ambaye
ni mkazi wa kwa Semtema akiwa na hali mbaya amelazwa chumba namba 9 lakini bado hali yake ni mbaya wala
hajapata ufahamu” alisema Tung’ombe.
Hata hivyo, licha ya
polisi kutaarifiwa alfajiri kabla ya saa 12 walifika katika eneo la tukio kwa
kuchelewa majira ya saa 02:37 asubuhi.
No comments:
Post a Comment