![]() |
| Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dk. Christine Ishengoma. |
Maafisa hao walijikuta katika wakati mgumu katika kijiji cha Chamndindi Kata ya Nyang’olo baada ya mwananchi aliyejitambulisha kwa jina Stanislaus Nziku kujitokeza mbele ya Mkuu wa Mkoa aliyekuwa katika ziara kijijini hapo na kuwatolea uvivu maafisa hao huku wananchi wakishangilia kwa makofi kumuunga mkono hoja ya mwenzao.
Wakati Ishengoma akiwa katika ziara katika vijiji vya Ikengeza, Chamndindi na Mangawe aliwataka wananchi kulima mazao ya muda mfupi nay ale yanayostahimili ukame ili kuepuka baa la njaa linaweza kujitokeza kutokana na ukame unaosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa.
Akizungumza na wananchi katika mikutamo ya hadhara Ishengoma aliwahimiza wananchi kulima mtama, viazi na mahindi ya muda mfupi kwa kufuata ushauri wa wataalamu hali iliyomlazimu mwananchi kuwatolea uvivu wataalam hao bila woga.
“Samhani, tumefurahi kusikia taarifa nzuri ya kilimo na kutueleza kuwa waataalamu wapo lakini mheshimiwa ukweli ni kwamba hawa wataalamu unaowasema huwa tunawaona kwenye misafara kama hii tu baada ya hapo
wanapotea moja kwa moja hadi kwenye msafara mwingine” alisema Nziku na
kushangiliwama na wenzake.
Ishengoma alipokea kwa masikitiko taarifa hiyo na kuwataka wananchi kutoa taarifa pale wataalam wasipoonekana wakati wa kilimo ili waweze kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria.
Aliwataka wananchi kutumia mbolea ya minjingu mazao ambayo huzalishwa hapa nchini ambayo inavirutubisho vya kutosha na kuongeza rutuba katika ardhi iliyochoka ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.
“Nawaomba sana wakati wa kilimo ukifika, tumieni mbolea ya minjingu mazao kwani ina virutubisho vyote katika kualishaji pamoja na kuongeza rutuba katika ardhi liyochoka ili muweze kupata mazao mengi kwa ajili ya chakula na biashara. Hii inatengenezwa hapa nchini” alisema Ishengoma.
Ishengoma amewata wazazi au walezi wenye watoto watakaopata nafasi ya kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza, wahakikishe watoto wao wanakwenda shule ili wakapae elimu badala ya kuwaoza kwa kutaka pesa.
“Matokeo ya darasa la saba yatatoka hivi karibuni, kwa hiyo ninawaomba wazazi na walezi wote wenye watoto watakaobahatika kujiunga na kidato cha kwanza wahakikishe watoto wao wanakwenda shule badala ya kuwazuia kwa lengo la kuwaoza kwa tama ya pesa” alisema.
Hata hivyo alisema kwa wale ambao hawatabahatika kujiunga na kidato cha kwanza wapelekwe katika vyuo mbalimbali vya ufundi ili waweze kupata elimu ya kujitegemea itakayowasaidia katika maisha yao.
“Wapo ambao hawatabahatika kujiunga na kidato cha kwanza, kwa hiyo wazazi nanyi walezi leo hii kuna vyuo mbalimbali vya ufundi, wapelekeni watoto wenu wakakapate elimu ya ufundi ili iwasaidie maishani mwao kwani wataweza kujiajiri wenyewe” alisema.
Katika hatua nyingine wenyeviti wa vijiji pamoja na maafisa watendaji walijikuta wakionja joto la jiwe baada ya wananchi kumuomba Mkuu wa Mkoa taarifa za mapato na matumizi juu ya michango yao ya ujenzi wa
shule.
Makaburi Kafuko mkazi wa kijiji cha Ikengeza ni miongoni mwa wananchi waliolalamika kuwa hawajawahi kusomewa mapato na matumizi ya ujenzi wa
shule yao ya Kata.
“Nashukuru sana kupewa nafasi hii adimu ili niweze kutoa dukuduku inayotutesa sisi wananchi. Tangu tuanze kuchangia ujenzi wa shule yetu ya kata, hatujawahi kusomewa mapato na matumizi. Sasa je, kuna haja gani ya kuendelea kuchangia wakati hatujui tumefikia wapi?” alisema na kuuliza Kafuko na kupigiwa vigelegele kama ishara ya kuungwa mkono na wenzake.
Katika ziara ya Mkuu wa Mkoa iliyohusisha vijiji vitatu, Ikengeza, Chamndindi na Mangawe alionesha masikitiko yake juu ya kujeruhiwa vibaya Mapadre wa Kaisa Katoliki Parokia ya Isimani na kuwataka wananchi kuwataja wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo ili waweze kuchukuliwa hatua za kiserikali.
“Mapadre wanajitoa sana kuwasaidia ninyi pamoja na kuleta huduma mbalimbali kwa ajili yenu lakini cha kushangaza mmewaumiza vibaya. Mlitaka kuwaua kwa sababu gani? Mlitaka wawafanyie nini ili mridhike? Taabia hiyo ife na muwataje wale wote wanaojihusisha na tabia hiyo ili tuwachukulie hatua za kisheria” alisema Ishengoma.

No comments:
Post a Comment