Watanzania wameaswa kutokubali ripoti ya kamati iliyoundwa
na Waziri wa Mambo ya ndani Emmanuel Nchimbi juu ya mauaji ya aliyekuwa
mwandishi wa habari wa kituo cha runinga cha Channel ten Daudi Mwangosi kwa
kuwa haina ukweli wowote na inapingana na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kauli imetolewa leo na Rose Mayemba mwanafunzi wa Chuo
Kikuu cha Ruaha (RUCO) katika umoja wa wasomi wa vyuo vikuu vya mjini Iringa
uliofanyika katika viwanja vya bustani ya Manispaa ya Iringa kwa ajili ya
kupinga ripoti hiyo na kulaani vitendo vya uongozi wa Mkoa huo kukaa kimya
baada ya tukio la mauaji ya mwanahabari huyo.
Mayemba amesema ripoti iliyotolewa na kamati ya nchimbi ni
batili kwa kuwa inalenga kuwaondoa wahusika wa tukio la mauaji hayo kwa
makusudi.
“Ripoti ya Nchimbi ni batili, inalenga kuwakwepesha
wahusika wa mauaji yale. Haikuwa na sababu yoyote ya kusomwa kwa kuwa haina
ukweli wowote. Inawapasa watanzania kuipuuza na kuilaani kwa kuwa inakiuka haki
za binadamu” amesema.
Pia mesem,a serikali kupitia vyombo vya dola hasa polisi
iache kuwalazimisha wananchi kufuata sheria zao feki zisizo za haki kwani
zinalenga ukandamizaji wa wazi.
“Serikali kupitia polisi acheni kutulazimisha kudfuata
sheria zenu feki za kikandamizaji na unyanyasaji kwani zinatunyima haki zetu
kwa makusudi. Hata hivyo Nchimbi alitumia sheria gani kuunda tumwe feki ambayo
imeleta ripoti feki namna hii” amesema.
Naye Olime Mwakilembe mwanafunzi wa RUCO amewataka serikali
kutumia ushahidi wa uhalisia ili kuwapa wananchi matumaini ya kupata haki zao
badala ya kupindisha uongo kuiwa ukweli kama
ilivyo kwa ripoti ya tume ya Nchimbi.
“Serikali iwe makini na ushahidi wa uhalisia, watumie picha
zinazoonesha ukweli badala ya kutumia uongo unaoonekana wazi. Huu ni uonezi na
ni udhalilishaji wa haki za binadamu” alisema Mwakilembe.
Amewataka wasomi waungane kwa pamoja katika kuishauri
serikali kuwa na ukweli kwa matukio ja kijamii badala ya kutumia mabavu na
uongo kwa kuiaminisha jamii uongo usio na maana.
“Wasomi tuwe na umoja katika kiishauri serikali kuwa na
ukweli kwa matukio kama haya ambayo
yanatudhalilisha bila sababu. Tunaipinga ripoti ya Nchimbi kwa sababu (1) ina
majibu feki, (2) haina uhalisia na (3) polisi wanalinda kibarua chao badala ya
kufanya kazi zinazostahili.
Jescar Kishoa mwanafinzi wa RUCO amewataka waandishi
kutokubali kulazimishwa kufanya kazi za kihuni kwa ajili ya kuwasafisha wahuni
na badala yake wawajibike kwa kufuata maadili yao.
“Waandishi msikubali kulazimishwa kuandika habari za
kuwasafisha watu waliojaa kila aina ya hila kwa ajili ya maslahi yao badala yake mfanye
kazi kwa kuzingatia maadili yenu kwa ajili ya manufaa ya jamii” amesema.
Vitus Rupeche mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini amewaasa
waandishi kuwa sauti ya wanyonge badala ya kutumika na mafisadi wasiokuwa na
huruma kwa wananchi na kufuata nyayo za marehemu Mwangosi wakati wa uhai wake.
“Waandishi msikubali kutumika na mafisadi na badala yake
muwe sauti ya wanyonge kama alivyokuwa
Mwangosi wakati wa uhai wake. Wanafunzi tulipokuwa tunadai pesa za mikopo,
Mwangosi alikuwa ndio sauti yetu na kuhakikisha tunapata mikopo hiyo.
Wasaidieni wanyonge” amesema.
Nico Mwakabilikile mwanafunzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha
Mkwawa amesema nchi inakoelekea ni kubaya kwa kuwa watu wachache wanaamua
kufanya mambo yao kwa maslahi yao binafsi bila kuwajali wengine.
“Nchi inakoelekea si kuzuri. Mauaji yanayoendelea kufanyika
yanatugawa wananchi katika matabaka kwa kuonesha upendeleo wa wazi. Alipouawa
Mwangosi mwandishi wa habari, serikali haikutoa matamko yoyote lakini alipouawa
kamanda wa polisi wa Mwanza, serikali imetoa matamko ya kila aina. Je, Mwangosi
hakuwa binadamu kama Liberatus Barlow? Huu ni
uonezi na matabaka haya hayafai kabisa” amesema Mwakabilikile.
Hali kadhalika Gofrey Bagamba mwanafunzi wa RUCO alisema
mwananchi wa leo si wa miaka ya 77 kwani ana upeo mkubwa wa mabo na kuyaona
mambo na kuyaelewa sambamba na kuujua uongo na ukweli.
“Sisi wananchi tunauona ukweli, hatuwezi kulazimishwa
kupotoshwa kuamini uongo wakati tunaona kwa macho yetu. Wananchi wa leo ni
tofauti na wale wa miaka ya 77 kwani tunayaona mambo na kuayelewa. Katiba ya
nchi inavunjwa na wachache wanaolazimisha mabo hasa serikali isiyokuwa na
mtizamo wa mbali kwa maslahi ya taifa” amesema Bagamba.
Katika hatua nyingine Oscar Kamayugi mwanafunzai wa Chuo
Kikuu kishiriki cha Mkwawa amelaani vikali vitendo vya uongozi wa mkoa wa
Iringa kukaa kimya katika tukio la kuuawa kwa Mwangosi kwa kujifanya kama mkoa hauna viongozi.
“Kitendo cha viongozi wa Mkoa kukaa kimya hadi leo katika
mauaji ya Mwangosi kilaaniwe kwa hali yoyote ile. Ni dhahiri kwamba serikali
inahusika kwa mauaji ya Mwangosi. Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa wilaya na viongozi
wengine wote walaaniwe. Ukimya wao unatuonesha wazi kuwa wao ni wahusika wakuu
na mauaji hayo waliyapanga kwa manufaa yao”
mesema Kamayugi.
Hata hivyo amesema vitendo wanavyoendelea kufanyiwa
waandishi wa habari wawapo kazini hasa katika kesi ya mtuhumiwa wa mauaji ya
Mwangosi vinafanyiwa kazi.
“Vitendo vya Polisi kupiga na kuwanyanyasa waandishi wa
habari waswapo kazini hasa mahakamani wanapoandika habari za mtuhumiwa wa
mauaji, sisi tunaviona na tunavifanyia kazi” amesema.
Amesema kuanzia leo watahakikisha waandishi wa habari
wanapiga picha za mtuhumiwa huyo kwa uhuru bila kubughudhiwa na mtu vinginevyo
patachimbika.
“Kuanzia leo hatutakuwa tayari kuona mtuhumiwa huyo
anafunikwa sura anapofikishwa mahakamani na hatutakuwa tayari kuona waandishi
wa habari wananyanyaswa wanapowajibika katika kazi zao vinginevyo patachimbika.
Amewataka wanairinga kushirikiana na waandishi wa habari
wakati mtuhumiwa huyo akifikishwa mahakamani ili kuhakikisha hafunikwi wala
waandishi hawafanyiwi hila yoyote.
“Umefika wakati sasa na sisi wananchi kuonesha machungu
yetu. Tuache shughuli zetu wakati mtuhumiwa huyo anapofikishwa mahakamani
kushirikiana na waandishi ili kuhakikisha anaonekana sura yake na waandishi
wanampiga picha bila bikumbo. Si kwamba hatuwezi, tunauwezo mkubwa sana, kwa nini waandishi
wanyanyashwe na sisi tukae kimya?” Tuoneshe nmachungu yetu.
Nicolas Francis amemtaka Kamanda wa polisi Mkoa wa Iringa
kwa hiari yake aondoke kwa kuwa wananchi wamechoka kumuona akiendelea
kurandaranda ndani ya mkoa huo.
“Nimpe taarifa Kamuhanda kwa hiari yake mwenyewe aondoke
Iringa kwa kuwa wananchi hawataki kumuona akiendelea kuzunguka na kurandaranda
mkoani hapa. Awaache wananchi wa Iringa warudishe amani yao
na waendelee na mahusiano yao
mazuri na p;olisi yaliyokuwepo hapo awali. Kamuhanda asiendelee kupandisha
hasira za wanairinga kwani asifikiri kwa kuwa wapo kimya wamemsifu kwa kile
alichokifanya. Kamuhanda uondoke kwa hiari yako” alisema.
Wasomi hao walipanga kuanza na maandamano kuanzia Kihesa na
kuhiotimisha katika viwanja hivyo vya bustani ya Manispaa lakini maandamano
hayo yalizuiliwa na Polisi hata hivyo w2asomi hao walifanya harambee kwa ajili
ya kumsaidia mjane wa marehemu Mwangosi.
No comments:
Post a Comment