masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Tuesday, October 2, 2012

Wananchi wa kijiji cha Utengule wamlilia Mwangosi

Hezlon Lusapi Mwenyekiti wa wanafunzi wa vyuo vikuu kutoka Wilaya ya Kilolo akiwahutubia wananchi katika kijiji cha Utengule

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Utengule wakisikiliza maelezo ya wanafunzi.





Mmoja wa wananchi wa akitoa rambirambi ya Mwangosi.


Wananchi wa Kijiji cha Utengule Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa wanaendelea kumlilia marehemu Daud Mwangosi kwa kutoa rambirambi ya shilingi 15,000 kwa ajili ya kusaidia mjane na watoto wake.

Hayo yalifanyika juzi katika mkutanao wa Chama cha Democrasia na Maendeleo CHADEMA uliofanyika na kijijini hapo na umoja wa wanafunzi wa vyuo vikuu wanaotoka katika Wilaya hiyo.

Akiwahutubia wananchi wa kijiji katika mkutano huo, mwenyekiti wa wanafunzi hao wilaya Hezlon Lusapi aliwataka wananchi kutokubali kuruzwa na viongozi  wasiopenda haki na kutumia nafasi zao kwa kuwaonea wengine.

“Msikubali kuwa watumwa wa viongozi wasio waadilifu na kuwatumia ninyi kama watumwa kwa ajili ya maslahi yao binafsi; hojini haki zenu bila woga ili muweze kupata ukweli wa jambo lolote” alisema Lusapi.

Alisema wapo baadhi ya viomgozi wanatoa amri kuwataka wananchi kuto michango bila kutolea maelezo juu y uhalali wa michango hiyo na matumizi yake.

“Kuweni na utamaduni wa kuhoji ukweli wa mambo, msikubali kuendeshwa kama magari mabovu kwa kuwa mna haki zenu za kujua kila kinachoendelea katika nchi na maeneo yenu kwa ajili ya maendeleo ya umma. Kuweni ni watu wa kuhoji na kujua uhalisia wa mambo” alisema.

Alisema wananchi wana jukumu la kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari wawapo kazini kwa kuhakikisha wanawajibika kwa manufaa ya umma.

“Kuuawa, kupigwa na kunyanyaswa kwa waandishi wa habari kunatokana na kukosa uongozi bora. Jamii tunajukumu la kutoa ushirikiano wa dhati kwa waandishi wanapowajibika kwa kazi zetu ili wawe salama kwa wakati wote” alisema.

Naye Oscar Ndale mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ruaha RUCO anayesoma kitivo cha sheria mwaka wa nne alisema ili kulijenga taifa la Tanzania, wananchi wasiwe kama wakimbizi ndani yao.

“Msikubali kuishi kama wakimbizi ndani ya nchi yenu, tunajua kuwa wapo baadhi ya viongozi wa wanaowajengea wananchi mazingira ya kuwa kama wakimbizi ili mradi wanyenyekewe kama watemi na kutowapa wananchi nafasi ya kuhoji. Wafichueni viongozi wa namna hiyo ili waweze kuwajibishwa” alisema Ndale.

No comments:

Post a Comment