masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Saturday, September 29, 2012

Wanaharakati wafanya Matembezi ya kumuenzi Daud Mwangosi leo

Wananchi walioamua kutembea kutoka Mafinga hadi Nyololo kwa ajili ya kumuenzi Daud Mwangosi na kulaani vitendo wanavyotendewa waandishi wa habari wakiwa kazini na jeshi la polisi Tanzania

Watembezi wakipumzika katika msitu wa Nyololo.

Watembezi wanapumzika katika stendi ya Nyololo bara baada ya kuwasili kijijini hapo.

Watembezi wakiwa wamesimama chini ya mti katika eneo alilouliwa Daud Mwangosi mara baada ya kupokelewa na wenyeji.

Mwenyekiti wa matembezi Mr. Bookshop alitoa ujumbe baada ya kupokelewa na wenyeji katika eneo hilo.


Ujumbe unavyosomeka katika fulana za watembezi hao

Mtembezi Selina Luhala akishindwa kutembea baada ya kuwasili katika eneo hilo.

Matembezi ya kumuuenzi aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha Channel Ten na Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Iringa (IPC) Daud Mwangosi yamefanyika leo kutoka mji mdogo wa Mafinga hadi Kijiji cha Nyololo alikouliwa.

Matembezi hayo ambayo yalikuwa ni mahususi kwa ajili ya kulaani vitendo wanavyotendewa waandishi wa habari wawapo kazini yalikuwa na ujumbe maalumu “WAANDISHI WA HABARI WAHESHIMIWE NA KULINDWA WANAPOCHUKUA HABARI”.

Kabla ya matembezi hayo watembezi walisema hakuna haja ya kumsubiri mtu kumuunga mkono kwa kuwa hata wakiwa wachache wanauwezo wa kufikisha ujumbe kwa jamii.

Matembezi ambayo yalikuwa ni ya watu watano ambao ni Mr. Bookshop, Rogers Mselu, Zacharia Zaheks, Muinjilisti Joisen Nyaluke wote wa Mafinga na Selina Luhala maarufu kwa jina la Mama Denis kutoka Iringa mjini ylipokelewa na Mwenyekiti wa kitongoji cha Ilala Nyololo njiapanda Shemu Kyando.

Akiongea mara baada ya kupokelewa kwa matembezi hayo mwenyekiti wa matembezi Mr. Bookshop wa Mafinga alisema wananchi hawanabudi kuwaaunga mkono waandishi wawapo kazini na kuwapa nguvu zaidi ili wasiwe na woga wakati wakiwajibika na kazi yao.

“Mwandishi wa habari ni mtu muhimu kwetu sisi wananchi kwa kuwa ndio watetezi wetu, tuwape nguvu za kutosha wawapo kazini ili wasiwe na woga wanapowajibika kwa ajili ya taifa letu” alisema.

Amewataka waandishi wa habari kutosaitiana katika msimamo wanaojiwekea ili kulinda nidhamu ya taaluma na heshima yao kwa jamii.

“Mwandishi ambaye ataonekana anaendelea kuandika habari za polisi wakati msimamo ni kutoandika habari za polisi, hatufai sisi wananchi na lazima tumtilie shaka juu yake na jeshi la polisi” alisema.

Alisema wakati zimebaki siku chache kufanya kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, wananchi wamekuwa hawana imani na usalama wao kutokana vitendo vichafu wanavyofanyiwa waandishi wa habari hasa kuuawa kwa Mwangosi na waandishi wa mkoa wa Iringa kuendelea kunyanyaswa na jeshi la polisi wanapowajibika kazini.

“Sioni haja ya kufanya kumbukumbu ya Mwalimu kwa sababu itakuwa ni kumdhalilisha tu. Yeye alipenda amani lakini amani hii imetoweka kwa vitendo vichafu, vya kinyama na vya kidhalimu vinavyofanywa na jeshi la polisi dhidi ya waandishi wa habari hususani waandishi wa Mkoa wa Iringa” alisema.

Watembezi hao waliotembea kilometa 41 wakati wakuwasilisha ujumbe huo, watembezi walioneshwa masalio ya nyama ya mwandishi huyo aliyeuawa kwa kufyatuliwa bomu Septemba 2, 2012.

No comments:

Post a Comment