masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Wednesday, September 26, 2012

Mmiliki wa mtandao huu anusurika kipigo kutoka kwa polisi

Askari wa kikosi cha kuzuia ghasia wakiwa wamesambaa mahakamani hapo kuwadhibiti waandishi wa habari.

Askari wakiwa wamejipanga mahakamani kuwazuia waandishi wa habari wasimpige picha mtuhumiwa.

Mikono ya Posili wakizuia waandishi kupiga picha.

Askari wakiwa katika mlango wa gari kumficha mtuhumiwa asipigwe picha.

Askari wakitoka mahakamani hapo mara baada ya mtuhumiwa kuondoka.







Mmiliki wa mtandao huu leo amenusurika kipigo kutoka kwa askari waliokuwa wameweka ulinzi mzito mahakamani wakizuia waandishi wa habari wasimpige picha mtuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa kituo cha televisheni cha Chanel Ten, Daud Mwangosi.

Hayo yametokea mara baada ya mtuhumiwa huyo Pasificus Alphonce Simon kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kwa mara ya pili.

Askari mwenye kitambulisho G.T. Timbuka katika mavazi yake alichukua uamuzi wa kutaka kumpiga mwandishi huyo baada mwandishi huyo kugundua mbinu iliyotumika kumfikisha mtuhumiwa huyo mahakamani hapo tofauti na siku ya kwanza alipofikishwa kwa gari la kifahari lenye namba za usajili T 320 ARC.

Tofauti na siku ya kwanza alipofikishwa kwa gari la kifahari, mtuhumiwa huyo leo amefikishwa mahakamani hapo kwa miguu na kupitishwa katika mlango wa nyuma wa mahakama ili waandishi wasimgundue mapema na kumpiga picha.

Mara baada ya mmiliki huyo kugundua njia hiyo na kutaka kuingia mahakani hapo alianza kusukumwa na askari na kupewa amri kuwa ni marufuku kuingia mahakamani hadi watakapotoa ruhusa ya kuingia.

Alipohoji ni utaratibu gani unatumika na ni lini umeanza askari aliyekuwa tayari kuanza kipigo aliyetambulika kwa jina la G.T. Timbuka katika vazi lake akiwa na kirungu mkononi akiambatana na askari waliovaa kiraia alisikika akisema “huyu anaonekana mbishi hajui kuwa anaweza kuwa kwenye mstari sasa hivi!”.

Wakati hayo yakiendelea walitokea askari wengine ambao walikuwa na silaha za moto na kutoa amri kwa mwandishi huyo kuondoka mapema eneo lile vinginevyo watamshughulikia.

Katika hatua nyingine mtuhumiwa wa mauaji hayo mwenye namba G 2573 akisomewa shitaka lake mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Dyness Lyimo, mwendesha mashtaka na wakili wa serikali Lilian Ngilangwa alisema mtuhumiwa huyo anatuhumiwa kwa kumuua Daud Mwangosi kwa makusudi mnamo tarehe 02.09.2012 katika eneo la kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa.

Mtuhumiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kisheria kusikiliza kesi za mauaji.

Ilielezwa kuwa upelelezi haujakamilika na kesi ikaahirishwa hadi Oktoba 10, 2012 itakapotajwa tena mahakamani hapo na mtuhumiwa amerudishwa mahabusu.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida askari wakiwa na magari madogo zaidi ya matatu na gari kubwa moja, mtuhumiwa huyo mara baada ya kutoka mahakamani alipakiwa katika gari lenye namba DFP 2175 Land cruiser Pic up.

No comments:

Post a Comment