| Balozi wa Marekani Alfonso E. Lenhardt akiwahutubia wnanchi wa Iringa |
| Balozi wa Marekani Lenhardt akihutubia |
Maambukizi ya Ukimwi Mkoni Iringa yanakadiriwa kuwa 15.6 % na ni ya juu kabisa nchini ambayo ni mara tatu ya wasatani wa Kitaifa.
Mradi
wa TUNAJALI rejea katika tiba jail afya yako umedhamilia kupambana na
maambukizi hayo pamoja na kutokomeza kabisa kufikia lengo la kuandikisha
na kasha kuwabakiza kwenye huduma na tiba za VVU/UKIMWI zaidi ya watu
20000 wanaoishi na virusi hivyo ili waweze kusihi maisha yenye afya na
tija zaidi.
Hayo
yamezungumzwa na Balozi wa Marekani Alfonso Lenhardt katika uzinduzi wa
mkakati wa “rejea kwenye tiba “ uliofanyika leo katika kituo cha Afya
Ipogolo Manispaa ya Iringa.
Alisema hivi sasa asilimia takribani 25% ya watu waliokuwa wakitumia ARV wameacha tiba hiyo ambayo ni muhimu na siyo tu kuwaanzishia watu dawa lakini ni muhimu pia kuhakikisha kuwa wagonjwa hao wanabaki katika tiba.
“Kiwango
hiki cha walioacha dawa kinatutia wasiwasi kuhusu afya na ustawi wa
watumiaji na pia kuhusu uwezekano wa kuongezeka kwa maambukizi katika
jamii kwa ujumla,” alisema Lenhardt.
Kwa
mujibu wa mwongozo wa huduma na tiba za VVU na UKIMWI uliofanyiwa
marekebisho na kutolewa na Serikali ya Tanzania mapema mwaka huu ambapo
kwa sasa mtu anastahili kuanza kutumia ARV wakati CD4 zake zikiwa 350 badala ya 200.
Alisema
uzinduzi wa Mkakati huo ni madhubuti kwa kueneza ujumbe wa “pima ,
endapo umeambukizwa na unastahili kuanza tiba ni vyema ukaanza mapema na
endapo umeacha tiba kwa sababu yoyote ile, ni lazima ukarejea kwenda
kupata huduma”.
| Baadhi ya wananchi wa Iringa waliohudhuria kwenye uzinduzi huo uliofanyika katika kiuo cha afya Ipogolo |
Aidha
Balozi huyo amesema katika kipindi cha miaka tisa toka 2003 watu wa
Marekani kupitia PEPFAR wamewekeza dola za Kimarekani Bilioni 2 kwa
ajili ya kupambana na VVU na UKIMWI nchini Tanzania ambao ni uwekezaji
katika maisha.
Kwa
mujibu wa taarifa ya mapambano dhidi ya Ukimwi Mkoani Iringa kwa
kipindi cha mwaka 2011/2012 ambapo Iringa imeathirika kwa kiwango
kikubwa ukilinganisha na Mikoa mingine Tanzania ambapo utafiti
unaonyesha maambukizi ya VVU na janga la UKIMWI kitaifa uliofanyika
mwaka 2007/2008 maambukizo yameongezeka kutoka asilimia 13.4% mwaka
2003/2004 na kufikia asilimia 15.7.
Aidha hatua ya mkakati huo imewezesha Watanzania zaidi ya 300,000 kutumia dawa zinazopunguza makali ya VVU ambapo hivi sasa zaidi ya Watanzania 525,000 hupokea matunzo na huduma mbalimbali zikiwemo huduma za majumbani.
No comments:
Post a Comment