Wednesday, October 3, 2012
Mtu asiyejulikana akutwa akiwa ameanguka na kuzimia Ngome
Mtu ambaye hakuweza kutambuliwa kwa haraka amekutwa akiwa ameanguka na kuzimia katika maeneo ya Kihesa Ngome ndani ya Manispaa ya Iringa.
Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 01:37 usiku ambapo kwa haraka mtu huyo hakuweza kutambuliwa na mtu yeyote licha ya watu wengi kukusanyika katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa baadhi ya mashuhuda waliohojiwa na mtandao huu walisema kuwa mtu huyo alipita akiwa anaendesha baiskeli yake na alipofika mbele kidogo gafla alipoteza mwelekeo na kuanguka.
Baada ya kutokutambuliwa na mtu yeyote, wasamalia wema walimkimbiza hospitalini japo kuwa haikueleweka wamemfikisha katika hospitali gani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment