masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Wednesday, October 3, 2012

Mbunge atoa chakula kwa wanafunzi wa shule ya Msingi

Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Ugele Fredrick P. Assenga akitoa shukrani zake kwa mwakilishi wa Mbunge Rose Mayemba jana ofisini kwake.

Mwalimu Mkuu Msaidizi Maurisia Shandu akiwa ofisini hapo.

Baadhi ya wanafunzi wa shule uya msingi Ugele wakihijiwa na waandishi wa habari shuleni hapo.

Baadhi ya wanafunzi wakiwa na mwakilishi wa Mbunge Rose Mayemba shuleni hapo.

Kulia ni mkazi wa Ugele Joyce Mkanila akishuhudia chakula kilichotolewa na Mbunge kikiwa katika ofisi ya Mwalimu Mkuu wa shule hiyo.

Mwakilishi wa Mbunge Rose Mayemba akiwa na wanafunzi shuleni hapo.

Walimu wa shule ya msingi Ugele wakiwa nje ya ofisi ya Mwalimu Mkuu mara baada ya kupokea chakula.


Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mch. Peter Msigwa (CHADEMA) ametimiza ahadi aliyoahidi kwa kutoa chakula katika shule ya msingi Ugele iliyopo katika kata ya Mtwivila Manispaa ya Iringa.

Kilo 100 za unga wa sembe pamoja na kilo 25 za maharage vilivyotlewa shuleni hapo vina thamani ya jumla ya shilingi 170,000/= ambapo shule hiyo ina waalimu wane akiwemo mwalimu wa kike mmoja.

Akikabidhi chakula hicho jana shuleni hapo, mwakilishi wa mbunge Rose Mayemba alisema huo ni mwanzo katika kuihudumia shule hiyo kwa kuwa yapo mahitaji mengine ambayo yatapelekwa kwa ajili ya wanafunzi.

“Mbunge amenituma nilete chakula hiki ikiwa ni sehemu ya ahadi yake kuwawezesha wanafunzi kupata chakula wakati wa masomo ili wasihangaike na kuhudhuria vipindi darasani kwa urahisi” alisema Mayemba.

Aliwataka waalimu pale linapojitokeza tatizo kuhusiana na shule hiyo, ofisi ya mbunge iarifiwe ili kupatiwa ufumbuzi.

“Matatizo yatakayo kuwa yanajitokeza yaelezwe kwenye ofisi ya mbunge ili yapatiwe ufumbuzi; pia iwe ni hamasa kwa wazazi kwa ajili ya kuwajibika na kutoa ushirikiano kwa Mbunge ili kuleta maendeleo” alisema.

Akipokea chakula hicho shuleni hapo, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Fredrick Assenga alisema Mbunge Msigwa amekuwa ni kiongozi wa utekelezji tofauti na viongozi wengine.

“Tumekuwa tukiahidiwa mara nyingi bila kutekelezewa lakini Mbunge Msigwa amekuwa tofauti na wengine kwa kuwa anaahidi na kutekeleza; hasa ukiangalia shule hii ambayo iko pembezoni kama huku, kwa kweli tuna kila sababu ya kumshukuru sana” alisema Assenga.

Aliwaomba watanzania wapende kuchangia kwa kuzisaidia shule zilizopo pembezoni kwa kuwa zimekuwa zikisahaulika kila wakati na wenye dhamana.

“Mimi naomba watanzania wapende kuchangia shule zilizo pembezoni kama hii kwa kuwa zimekuwa zikisahaulika kila wakati na wenye dhamana ya kutoa huduma hasa viongozi wa serikali. Naamini kuna wadau mbalimbali ambao wanaweza kuguswa na kusaidia kwa ajili ya maendeleo” alisema.

Naye Joyce Mkanila mkazi wa Ugele alisema wakati umefika kwa wananchi kuangalia nani muongo na nani mkweli ili waweze kuchukua maamuzi sahihi wakati wa uchaguzi ukifika.

“Tumekuwa tukilalamika kuwa Mbunge ametudanganya lakini sasa hatutasema tena. Vile vile nawasihi wananchi wenzangu kuangalia nani muongo na nani mkweli ili kufanya uamuzi sahihi siku ya uchaguzi ukifika” alisema Mkanila.

No comments:

Post a Comment