masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Wednesday, October 3, 2012

Waandishi wa habari Iringa wafumbuliwa macho

Deodatus Balile akiwaelimisha waandishi wa habari wa Mkoa wa Iringa juu ya maadili ya habari.

Balile akiwa na Rose Ngunangwa wakati wa mafunzo.

Laurian Mkumbata akiwasilisha kazi baada ya majadiliano katika vikundi.

Rose Ngunangwa akielekeza kwa vitendo wakati wa mafunzo.


Waandishi wa habari Mkoa wa Iringa wamefumbuliwa macho kwa kutakiwa kuwatumia wanasheria kuishitaki serikali juu ya kuuawa kwa mwandishi wa habari wa kituo cha runinga cha Channel Ten Daud Mwangosi.

Hayo yamezungumzwa leo na Deodatus Balile katika ukumbi wa maktaba ya Mkoa huo ikiwa ni siku ya mwisho ya mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya maadili ya uandishi.

Balile alisema kila mtu ana haki, na endapo atakwenda kinyume na taratibu anatakiwa kuchukuliwa hatua za kisheria.

“Ni haki yenu kuwatumia wanasheria kuishtaki serikali juu ya kifo cha mwanahabari mwenzenu kwa kuwa aliuawa wakati akiwajibika katika kazi yake. Ni haki yenu kuishtaki serikali ilipe fidia kwa kuwa si haki mtu kuuawa wakati akiwajibika katika kazi yake bila sababu yoyote” alisema.

Alisema nchi yoyote duniani inaongozwa kwa sheria na kanuni na pale inapoonekana mtu anavuvya taratibu hizo anatakiwa kuchukuliwa hatua za kisheria ili aweze kukumbushwa wajibu wake.

“Nchi yoyote duniani inaendeshwa kwa kwa sheria, kanuni na taratibu na pale anapoonekana anakwenda kinyume na taratibu hizo anatakiwa kuchukuliwa hatua ili akumbushwe wajibu wake lakini kwa kuuawa kwa mwanahabari mwenzenu haikustahili kuwa hivyo kabla ya kutiwa hatiani; serikali inabidi kuwajibika kwa hilo moja kwa moja na kuwajibika kuitunza ile familia” alisema.

Alisema kukatishwa uhai kwa mtu akiwa katika nafasi yake ya kazi ni kinyume cha haki za binadamu na ni ukiukwaji wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayompa mtu uhuru wa kuishi.

“Kitendo alichofanyiwa mwanahabari mwenzenu ni cha ukiukwaji wa haki za binadamu na ni kinyume na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayompa mtu haki ya kuishi. Kama angekuwa na kosa alitakiwa kuchukuliwa hatua za kisheria na si kuhukumiwa bila kupewa nafasi ya kujieleza na kujitetea” alisema Balile.

Wakati huo huo Rose Ngunangwa aliwataka waandhishi kutumia maadili yao ipasavyo ili kuijenga jamii yenye nidhamu na heshima katika uwajibikaji.

“Wanahabari mkitumia maadili yenu mtaijenga jamii yenye nidhamu na heshima katika uwajibikaji na kufanya kazi kwa maslahi ya umma na kuacha ubinafsi unaoweza kusababisha uhasama ndani ya jamii na taifa kwa ujumla” alisema.

Hali kadhalika wahariri  na wamiliki wa vyombo vya habari wametakiwa kutoa ushirikiano kwa waandishi ili kulinda maadili ya habari na vyombo vya habari kwa ujumla.

“Wahariri na wamailiki wa vyombo vya habari nao wanatakiwa kutoa ushirikiano wa hali ya juu kwa waandishi wao ili kulinda maadili ya habari na vyombo vya habari kwa ujumla” alisema.

Mafunzo hayo yalikuwa ya siku tatu kuwajengea uwezo wa kimaadili waandishi wa habari kutumia maadili yao katika uwajibikaji wao.

No comments:

Post a Comment