| Deogratius Mfugale mwezeshaji wa mafunzo ya uandishi wa habari za mazingira akiwa mbele ya wanahabari katika chumba cha mafunzo. |
| Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya uandishi wa habari za mazingira |
WAANDISHI wa habari nchini wametakiwa kuandika habari za mazingira ili kuieleza jamii changamoto mbalimbali za uharibifu unaojitokeza katika maeneo mbalimbali nchini na duniani kwa ujumla.
Kauli hiyo imezungumza leo na Deogratius Mfugale mwezeshaji wa mafunzo ya uandishi wa habari za mazingira yanayoendelea mkoani humo kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa uandishi wa habari za mazingira.
Mfugale amesema miongoni mwa mambo yanayokwamisha habari za mazingira ni kutokuwa na nyenzo muhimu zinazowawezesha waandishi kuwajibika ikiwa ni pamoja na serikali yenyewe kutolipa suala la mazingira kipaumbele.
Ili kukabiliana na suala la uharibifu wa mazingira waandishi wametakiwa kujituma kuikumbusha jamii kwa kuwa ndiyo waathilika wa kwanza wa mazingira yanapoharibika.
“Waandishi wa habari mmekuwa hamuandiki habari zinazohusu mazingira na hii ni sababu moja kubwa ambayo inachangia mazingira kuendelea kuharibika siku hadi siku; jamii ikikumbushwa mara kwa mara itawajibika ipasavyo” alisema.
Amesema serikali kwa kusaidia na wadau mbalimbali wa mazingira wananafasi kubwa kuwawezesha waandishi katika kuandika habari hizo hali ambayo imesahaulika na mazingira kuendelea kutelekezwa siku hadi siku.
“Serikali kwa kusaidiana na wadau mbalimbali wananafasi kubwa ya kuihamasisha jamii katika utunzanji wa mazingira kwa kupitia waandishi wa habari lakini serikali na wadau wamekuwa wakilisahau suala hili kana kwamba si la muhimu” alisema.
Aidha amesema kutokana na kukosekana kwa elimu juu ya mazingira, binadamu ambaye ni muathirika wa wa kwanza kunaendelea kuleta wasiwasi juu ya uwajibikaji wa dhati katika kutekeleza utunzaji wake kwa manufaa ya viumbe vyote hai.
Mafunzo hayo yameandaliwa na umoja wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) kwa kufadhiliwa na SIDA kuanzia Oktoba 17 hadi Oktoba 20 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment