Mohamed Enterprises inayojishughulisha
na uuzaji wa pembejeo za kilimo pamoja na bidhaa mbalimbali nchini imenyang’anywa
leseni hiyo na mamlaka ya udhibiti wa mbolea nchini - Tanzania Fertilizer
Regulator Authority (TFR) iliopo chini ya wizara ya kilimo, chakula na ushirika
baada ya kuvunja masharti ya uuzaji wa mbolea.
Akizungumza na mtandao huu hii leo Mkurugenzi mtendaji wa TFRA Dk. Susan Ikerra, amesema hatua hiyo
imetokana na kampuni kuvunja taratibu za biashara ya mbolea na hivyo wakulima
kuingia hasara kwa kuuziwa pembejeo zilizo mbovu.
Dk. Ikerra amesema makosa yaliyosababisha kampuni hiyo kunyang’anywa na kufungiwa biashara
ya mbolea nchini, ni pamoja na bidhaa hiyo kukutwa ikiwa haina vigezo
huku mbolea ya CAN na DAP kuwa na virutubisho vya Nitrojen 12 kati ya 27
inayotakiwa jambo linaloifanya mbolea hiyo kutofanya kazi inayokusudiwa.
“Kampuni hii
imevunja masharti ya uuzaji wa mbolea nchini, anauza mbolea iliyo na ujazo wa
kilo 9, hatuna ujazo huu sisi, hiyo haikubaliki, pia mbolea hii imegnda kama
aunavyoona, tayari imepoteza ubora wake, kwa hiyo mkulima akinunua mbolea hii
haitamsaidia, huu ni uchafu tu, na nimenyang’anya leseni yake kwa sababu hizo,
afanye biashara nyingine, lakini siyo ya mbolea,” amesema Dk. Ikerra
Amesema
lengo la mamlaka hiyo licha ya kuanza mapema mwaka huu itahakikisha mbole
inayouzwa kwa mkulima inakuwa na ubora ili kuboresha sekta ya kilimo, kwa
kuondoa uchafu na changamoto zinazowakabili wakulima na kuwapa hasara bada ya
kuuziwa mbolea zisizofaa.
“Nimekuja
Iringa kuhakiki ubora wa mbolea kwenye magodawn, kwenye maduka, na kwa
mawakala, ambako huko nimekuta matatizo makubwa kama uwepo wa mbolea
zisizo na taarifa maalumu kutengenezwa wala kuisha muda wake, mbolea nyingi
zimeganda na tayari nimemjulisha mkurugenzi wa kampuni hii, na amekubaliana nami,” amesema.
Amesema
matokeo ya maabara kutoa SUA juu ya mbolea hiyo kutokuwa na ubora tayari
yalikabidhiwa kwa Waziri wa kilimo mwenye dhamana Christopher Chiza, huku
naye Mohamed Enterprises akipatiwa taarifa hiyo pamoja na barua ya usitishaji
wa biashara hiyo.
Ameutaka
uongozi wa kampuni hiyo kutouza mbolea hiyo ya CAN na DAP, kwani amefungiwa
rasmi kufanya biashara hiyo, na kuwa jeshi la polisi na Manispaa zitapewa barua
ya sitisho la leseni ya uuzaji wa mbolea kote nchini.
Naye ofisa
kilimo wa Manispaa ya Iringa Gerald Mwamuhamila amesema baada ya kubaini kampuni
hiyo inawauzia wakulima mbolea chafu walifika katika ghara hiyo na kukuta
mifuko ya mbolea isiyo na naironi ya ndani, jambo linalosababisha mbolea
kupoteza ubora mapema.
Mwamuhamila
amesema katika ghara hilo kulikuwa na mbolea zilizokuwa zimeganda, huku kukiwa
na mifuko ya mbolea aina ya UREA yenye ujazo wa kilo 9 ambayo haifahamiki,
kwani hakuna ujazo huo na kuchukua baadhi ya mifuko hiyo kama ushahidi na
kuipeleka polisi.
Mtaslimu
(Accountant officer) wa kampuni ya Mohamed Enterprises mkoa wa Iringa Ivan Ole
Mganga alikubaliana na hatua hiyo na kuweka saini katika fomu ya usitishwaji wa
leseni katika biashara hiyo ya mbolea.
Nao baadhi ya mawakala wa mbolea,
walikutwa na zoezi hilo wakikiuka taratibu za utunzaji na uuzaji wa mbole, huku
wengi wao wakiwa wameifungua mifuko hiyo ya mbolea jambo lilipunguza ubora na
kuyafanya mazao yashindwe kustawi vizuri.
Akitoa sababu za kufanya hivyo mmoja wa
wauzaji wa bidhaa hiyo Charles Kamazu alisema hulazimika kufungua mifuko kwa
lengo la kupima kwa ujazo wa kilo, kwani baadhi ya wakulima hwana uwezo wa
kununu mfuko mzima wenye kilo 50.
Mawakala nao waliiomba serikali kuweka
mbolea hiyo pi katika ujazo wa kilo 2 na zaidi ili kuwasaidia wananchi hao,
kwani walio wengi wamekuwa wakinunua mbolea kidogo kidogo pasipo kujua madhara
yake.
“Hatufahamu kama mfuko ukifunguliwa na
kuachwa wazi mbolea inakwisha ubora, lakini tunalazimkka kufany hivyo kwani
wateja walio wengi ndiyo wanataka kupimiwa kuanzia kilo moja na kuendelea,
serikali ianzie kufunga mbolea kuanzia kilo mbili siyo mbaya,” mesema Kamazu.
Pia waliitaka serikali kutoa elimu zaidi
juu ya utunzaji wa pembejeo hizo, ili kuepukana na uharibifu wa bidhaa hiyo,
unaosababisha ubora kupungua, na kumsababishia mkulima hasara na hivyo sekta ya
kilimo kushindwa kufikia mlengo yake.
Wakati wa
uanzishaji wa mamlaka hiyo mapema mwezi wanne, waziri Chiza alisema, TFRA
imeanzishwa ili kusimamia masuala yote yahusuyo sekta ya mbolea na ubora
wake-Bio, ambapo kutakuwa na utaratibu wa ukaguzi wa mara kwa mara wa bidhaa
hiyo.
|
Sunday, October 28, 2012
MOHAMED ENTERPRISES YANYANG’ANYWA LESENI NA TFRA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment