masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Sunday, September 2, 2012

Mwenyekiti wa Iringa Press Club auawa Habari zilizojitokeza sasa hivi

Katikati ni Mweyekiti wa Iringa Press Club Daudi Mwangosi aliyesimama ni Katibu Mkuu wa IPC na kusho Mwekahazina wa IPC Selemani Boke

Habari zinazotufikia sasa zinasema Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Iringa (IPC) Daudi Mwangosi ameuawa na jeshi la polisi katika mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendelo CHADEMA dakika chache zilizopita.

Chadema walikuwa katika harakati za operesheni sangara maarufu kama M4C katika Wilaya ya Mufindi katika mkoa wa Iringa.

Mwangosi ambaye pia ni mwandishi wa habari wa Chanel 10 aliongozana na msafara huo kwa ajili ya kuandika habari.

Kwa mujibu wa Mwandishi wa habari wa Radio Free na Star TV Oliva Motto amezungumza na mtandao huu kwa njia ya simu na kuthibitisha kuwa jeshi la polisi wamemua Mwangosi kwa silaha ya moto huku wakiwageukia waandishi kuwataka wasiandike habari za chama hicho.

"Vita imewageukia waandishi wa habari kututaka tusiandike habari zozote kuhusu Chadema na hivi sasa tumejificha porini hatujui lakufanya" amesema Motto.


ENDELEA KUFUATILIA HABARI HIZI

No comments:

Post a Comment