masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Sunday, September 2, 2012

Iringa kwanukia machafuko

Mkurugenzi wa mipango na mafunzo wa Chadema Benson Kigaila akiongea na waandishi wa habari

Benson Kigaila akiwaonesha waandishi wa habari kibali walichopewa na jeshi la polisi jana kuruhusu mikutano.


Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Slaa akizungumza na waandishi wa habari

Dk. Slaa akizungumza

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Dk. Willibrod Slaa chama chake hakitaacha kazi ya operesheni sangara kwa sababu ya matakwa ya watu binafsi.

Amesema haya leo katika mazungumzo yake na waandishi wa habari mjini Iringa akisisitiza kuwa chama chake hakitakuwa tayari kutimiza matakwa ya watu wachache vinginevyo kikifutiwa usajili.

Kauli ya Dk. Slaa imekuja siku moja baada ya jeshi la Polisi mkoa wa Iringa kusitisha mikutano ya chama hicho kwa mara ya pili wakisingizia kuwa zoezi la sense linaendlea nchini na kutaka isifanyike mikutano yoyote.

“Chadema haitaacha kazi hiyo labda ifutwe kwenye vitabu vya usajili. Hali hii haiwezi kuvumilika kwa sababu ni watu wachache wanaotaka tutii matakwa yao, tuna haki ya kikatiba na kisheria kufanya mikutano hii nchini lakini jeshi la polisi linatoa maagizo haya kwa matakwa yao binafsi” alisema Dk. Slaa.

Kwa mujibu wa  Mkurugenzi wa mipango na mafunzo wa Chadema Benson Kigaila, jeshi la polisi lilitoa kibali jana asubuhi kuruhusu Chadema kufanya mikutano kama walivyopanga na ilipofika saa 10 za jioni wakatoa barua ya kusitisha mikutano hiyo.

“Walipositisha mikutano yetu kwa mara ya kwanza walisema baada ya siku 4 za sense tutaendelea nas operesheni yetu tukakubali kwa busara japo ilikuwa kutimiza matakwa ya jeshi hilo na si sheria. Jana asubuhi tulipewa kibali cha kuendelea na na mikutano yetu lakini ilipofika saa 10 jioni tukapewa barua ya kusitisha mikutano kwa kisingizio kilekile. Hatuwezi kulifumbia macho suala hili” alisema Kigaila.

Dk. Slaa alisema umefika wakati ambao dunia inataka kujua kinachotokea Tanzania kama ni cha kidemokrasia na kutoa majibu ni nani anakosa busara kwa kutumia mabavu badala ya demokrasia.

“Sisi Chadema daima ni wapole lakini je, upole wetu utakoma lini? Sisi ni wavumilivu sana lakini nataka kujua uvumilivu wetu utakoma lini? Sisi tunapenda kutumia busara lakini hii busara itumike mpaka lini wakati tunaendelea kuumia na kuonewa?” alisema Dk. Slaa.

Amelitaka jeshi la polisi kuueleza umma kuwa ni sheria ipi imevunjwa badala ya kutumia nguvu ya kuzuia mikutano ya hadhara inayofanyika kwa amani.

“Jeshi la polisi watuambie ni sheria ipi inavunjw badala ya kutumia nguvu. Uonezi hauvumiliki duniani kote, tunataka Dunia nzima ijue haya kuwa Chadema haina nia mbaya” alisema.

Alisema kuwa alipowasiliana na IGP Said Mwema jana kwa njia ya simu, Mwema alimwambia kuwa wametoa maagizo kusitisha mikutano wakati sense inapoendelea kufanyika nchini bila kueleza ni sheria ipi imetumika kutoa maagizo hayo na sitisho hilo.

“Tunatambua kuwa sheria ya sense inawahusu wale ambao watakataa kutoa taarifa zao au kuhesabiwa lakini si kuathili shughuli zozote za kijamii na za maendeleo kwa taifa” alisema.

Akisimulia jinsi walivyoaanza kupa misukosuko ya kutaka kusitisha shughulizo mkoani Morogoro alisema kuwa Jeshi la Polisi walitoa visingizio vinne ambavyo vilikuwa ni vya kipuuzi ambavyo kikiwepo cha kuwepo na mikutano ya CCM katika viwanja walivyoviomba wao kufanyia mikutano, Kuwepo nanenane mkoani humo, mgomo wa walimu unaoendelea nchini pamoja na barabara ya Morogoro kuwa finyu.

Chadema ilipanga kufanya mikutano kuanzia 28 Agosti katika mkoa wa Iringa na kusitishwa na jeshi la polisi kupisha zoezi la sensa jambo ambalo lilikuwa vuta nikuvute katika ya Chama hicho na jeshi la polisi.

No comments:

Post a Comment