| Dr. Willibroad Slaa akiongea na vyombo vya habari. |
| Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Willibroad Slaa Kushoto na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Saidi Isa Mohamedi wakiongea na vyombo vya Habari leo |
| Kingo Kigaila Benson mratibu wa operesheni Sangara akiongea na vyombo vya habari leo. |
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Dr. Wilibroad Slaa amemtaka Spika wa Bunge mstaafu Samwel Sitta kuacha unafiki na na badala yake kujenga hoja zenye maslahi kwa taifa.
Dr. Slaa ameyasema haya leo kwa vyombo vya Habari katika umbi wa M.R. Hotel Mjini Iringa akimjibu Sitta juu ya hoja yake kuwa Chadema ina viongozi wa wanaojua kuchezesha disco na si uongozi wa serikali katika faita.
“Sitta ni mnafiki, muongo, mzushi na mbinafsi; tulitegemea mtu mstaarabu, msomi kutoa hoja za akili kumbe anarudi kwenye uchafu uleul. Sitta ni mtu ambaye hna hata uti wa mgongo” alisema Dr. Slaa.
Amemtaka Sitta akamlize migogoro ndani ya chama chake yaliyokithiki na kuwagawa katika makundi huku wakiendelea kulitafuna taifa na aache mara moja kuzungumza juu ya chama kingine ambacho kina tartibu na viongozi wake.
“Namsihii Sitta akamalize migogoro na matatizo ya chama chake na aache kuzungumza juu ya chama hkingine ambacho kina taratibu zake na viongozi wake, aache upuuzi na afahamu kuwa hakuna chuo chochote kinachofundisha Siasa” alisema.
Sitta amepaswa kufahamu kuwa wacheza disco ni wapiga kura na wapo hata mawaziri wa chama cha mapinduzi wanaokesha katika ukumbi wa Bilikana wakicheza disco hiyo hiyo anayosema haifai na pia ametakiwa kujua kuwa kumbi kama hizo zipo kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.
“Kitendo cha Sitta kuizungumza Chadema badala ya chama chake ni kuthihirisha kuwa Chadema inatisha. anataka kuliambia taifa kuwa wacheza disco ni wadhambi. Nimkumbushe kuwa wacheza disco ni wapiga kura na wapo mawaziri wa CCM wanaokesha katika ukumbi wa Bilikana wakicheza disco. Mbona hao hasemi? Sisi Chadema tunautaratibu wetu wa kuchagua viongozi, asitupangie” alisema.
Dr. Slaa amesema Sitta ni mhaini kwa kile alichosema maneno yake hayaendani na kile anachokisema kwa jamii na hana ujasiri wa kufanya maamuzi.
“Sitta ni mhaini, ndiye mwanzilishi wa Chama cha Jamii CCJ. Sitta alipotolewa na kamati kuu ya chama chake NEC aliomba kugombea uspika kupitia Chadema akidai kuwa ana wbunge zaidi 55 wa CCM ambao yeye akihama chama atahama nao lakini alipoambiwa atangaze kukihama chama alikimbia na kuzima simu kabisa. Sitta tulipanga kwa pamoja kuwa angegombea urais kupiti Chadema lakini baada ya kuona ni muongo tuliachana naye” alisema Dr. Slaa.
Alisema kuna watu wanajiona ni wasomi kumbe ni mbumbumbu kuliko watu wote na ndiyo maana nchi inayumbishwa na mafisadi bila kuchukuliwa hatua zozote za kisheria ambazo zingekomesha tabia hiyo.
“Sitta asijione ni msomi kumbe ni mbumbumbu kuliko watu wote, ni dhahiri kuwa hajui sheria zanchi ni Waziri asiyejua majukumu yake na badala yake anaendekeza uongo, unafiki na uzushi kwa jamii” alisema.
Pia Dr. Slaa amesema Sitta hana uadilifu kwani nifisadi zaidi ya mafisadi wenyewe ambao wanalitafuna taifa kwa kuiba mali za umma na kujilimbikizia wao na familia zao.
“Sitta anauadilifu gani katika nchi hii? Alijenga ofisi ya spika huko Urambo, alijenga nyumba yenye thamani ya shilingi milioni 300. Mimi nauliza kuna spika gani huko Urambo? Richmond ambayo mpaka leo haina majibu aliyefunga mjadala ni Sitta. Alifunga hoja kwa sababu ya kuilinda CCM. Watu wa CCM tunawajua kila mmoja tutawaumbua mmoja mmoja” alisema na kuhoji Dr. Slaa.
Amemtaka Sitta kama anaujasiri ajitokeze hadharani kujibu hayo na kwamaba Chadema hawapendi kumzungumza mtu lakini wakichoko zwa hawatamfumbia mtu macho huku akisema hayo ni baadhi tu ingawa yapo mambo mengi yanayomhusu Sitta ambayo ameyaacha.
Wakati huo huo makamu Mwenyekiti wa Chadema taifa Said Issa Mohamed amewataka waislamu kutokubali kutumiwa na chama cha Mapinduzi kwa propaganda chafu wanazozifanya kwa kutumia udini katika siasa.
"Nawasihi sana ndugu zangu waslamu msikubali kutumiwa na chama cha mapinduzi kilichofilisika kifikra na kutumia udini kwa madai ya Chadema ni chama cha wakristo, wapuuzeni hao kwani wanawatumia ninyi kwa maslahi yao binafsi" alisema Mohamed.
Amesema kuwa kuna baadhi ya watu wanatumia ujumbe mfupi kwa kuwashawishi waslamu wasijiunge na Chadema kwa madi kuwa ni chama cha wakristo jambo ambalo ni hatari katika taifa.
"Kuna watu wanatuma ujumbe mfupi kuwashawishi waislamu wasijiunge na Chadema kwa madai kuwa ni chama caha Wakristo jambo ambalo ni hatari kwa taifa. Nawaomba waislamu wenzangu msikubali huo ni uzushi kwa kuwa mimi mwenyewe ni muislamu pia na nina msikiti na ninaendesha madrasa kama kawaida nikiwa kama Makamu Mwenyekiti wa Chama" alisema.
No comments:
Post a Comment