| Milango ya Maktaba ya Mkoa wa Iringa ikiwa bado imefungwa saa 3 asubuhi. |
| Mlinzi wa ofisi hizo akifungua milana saa 3:37 asubuhi. |
| Ofisi ya Mkutubiwa wa maktaba hiyo ikiwa haijafunguliwa. |
| Moja ya choo kinachotumika na watu mbalimbali wanaofika kupata huduma katika Maktaba hiyo. |
Wakati serikali ikiwa katika mkakati wa kuwachukulia hatua wafanyakazi wa umma wanaotuhumiwa kwa kashfa mbalimbali, baadhi ya ofisi za umma zinachelewa kufunguliwa katka muda unaotakiwa.
Waandishi wa habari wa Mkoa wa Iringa ambao wako katika mafunzo ya uandishi wa makala unaofanyika katika ukumbi wa maktaba ya mkoa, wameshindwa kuanza vipindi kwa muda mwafaka kutokana na ofisi za Maktaba hiyo kutokuwa wazi wakati wa asubuhi.
Ikiwa leo ni siku ya pili kwa waandishi kushindwa kuanza vipindi kwa muda, juzi walichelewa kuanza kutokana na kukosa vifaa vya kufundishia baada ya ofisi ya mkutubi wa maktaba hiyo kutofunguliwa hadi saa saba za mchana alipotokea ofisini.
Baada ya waandishi kufuatilia shida iliyojitokeza hadi mkutubi huyo kuchelewa, wahudumu walishindwa kueleza kilichotokea kwa madai kuwa hawajui hata walipojaribu kutafuta simu yake ya mkononi kutopatikana.
Siku iliyofuata waandishi walijikuta wakikaa nje kutokana na ofisi kuendelea kufungwa hadi saa 03:37 asubuhi zilipofunguliwa na mlinzi wa zamu bila kutolewa nini kimesababisha.
Mara kadhaa waandishi walikuwa na shauku ya kumuona muktubi wa maktaba hiyo ili kujua ni utaratibu gani unatumika kufunguliwa kwa ofisi hizo lakini ofisini alikuwa hapatikani hadi ilipofika saa 8 za mchana alipotokea ofisini kwake.
Alipofuatwa na waandishi ili kutolea maelezo juu ya jambo hilo muktubi wa Maktaba hiyo ya Mkoa Hilida Kapusi hakuwa tayari kuwapokea waandishi hao kwa kile alichoeleza kuwa hawapendi waandishi wa habari.
“Kwani kuna nini? Unajua mwenzenu siwapendi waandishi wa habari wala siwahitaji. Siwezi kuzungumza nao lolote” alisema Kapusi.
Alipotakiwa kueleza ni kwa nini hawapendi waandishi wa habari hakuwa na sababu zozote kwa kile alichosema hawapendi tu.
“Mimi siwapendi tu. Si kwamba kuna sababu zozote bali tu roho yangu haiwapendi na huwa sipendi hata kuwaona” alisema.
Sambamba na hilo vyoo vinavyotumika na watu mbalimbali wanaofika kupata huduma katika maktaba hiyo haviridhishi kutokana na uchafu uliokithiri.
Ukumbi huo hukodiwa kati ya shilingi 50 na laki moja kwa wahitaji wanaotaka kutumia.

No comments:
Post a Comment