![]() |
| Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete |
Taarifa zinazotufikia sasa zinaeleza kuwa Jeshi la Wananchi (JW) limetumika katika mkutano wa Chadema huko Mufindi kuhakikisha lolote linafanyika katika kuzuia vuguvugu la mabadiliko M4C kufanyika.
Kauli ya jeshi la polisi Mkoa wa Iringa ilieleza kwamba, jeshi hilo limejipanga kwa namna yo yote kuhakikisha mkutano wa Chadema haufanyika popote.
Kutokana na kauli hiyo wadau mbalimbali na wanaharakati wanalaani vikali jeshi la polisi kutumia nguvu badala ya kutumia njia ya amani.
Itakumbukwa kuwa Kamuhanda alipokuwa katika mkoa wa Ruvuma aliamrisha askari wake kua wananchi walioandamana kupinga mauaji ya kinyama ya wanawake na kukatwa viungo vyao vya mwili ikiwa ni wanawake 9 waliuawa.
Kijana mmoja alikufa baada ya kushambuliwa na jeshi la polisi huko mkoani Ruvuma kupinga mauaji ya wanawake hao.
Katika tukio la leo litakuwa la kwanza baada ya Kamanda Kamuhanda kuanza kazi yake katika mkoa wa Iringa huku likiwa la mara ya pili kwake akiwa RPC ambapo la kwanza lilifanyika Mkoa wa Ruvuma baada ya mwananchi kuuawa na askari wakipinga maauaji ya wanawake.
Licha ya Chadema kukataliwa kufanya mikutano ya hadhara Chama cha Mapinduzi CCM kinaendelea kufanya mikutano katika Kata ya Idete Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa ambapo jana walifanya katika kijiji cha Madege.

No comments:
Post a Comment