| Michael Kamuhanda |
MAANDAMANO ya kumhamisha kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda yanaandaliwa na Mbunge wa jimbo la Iringa Mjini, Peter Msigwa.
Kauli hiyo imetolewa na Msigwa leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake akisikitishwa na vitendo vichafu vinavyofanywa na jeshi la polisi nchini.
Msigwa amesema hamasa hiyo inatokana na hatua ya kiongozi huyo kushindwa kuwajibika, pale yalipotokea mauaji ya mwandishi wa habari wa Chanel Ten ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa habari Mkoani Iringa (IPC), Dauidi Mwangosi.
Amesema ni jambo la kushangaza kwa kiongozi ambaye anashindwa kuwalinda waandishi wa habari wakiwa kazini na badala yake kuhamasisha mauaji ya makusudi kwa watu wasio na hatia.
“Ni jambo la kushagaza kuona kiongozi ambaye alishindwa kuwalinda waandishi wa habari wakiwa kazini, na kusababisha mauaji akiendelea kuvaa magwanda na kuingia ofisini kwake kama
Sambamba na hilo
amewata wananchi wa Iringa kutojitokeza katika wiki ya usalama barabarani hadi hapo viongozi wa serikali watakapotoa kauli ya kulaani mauaji ya Mwangosi.“Naamini wananchi wengi wameguswa na mauaji ya Mwangosi. Ninachowataka wananchi wakati wanapoendelea na maombolezo haya, wasijitokeze katika wiki ya usalama barabarani hadi hapo viongozi wa serikali watakapotoa kauli ya kulaani mauaji ya Mwanosi, ambayo yametokea hivi karibuni kwenye eneo la Nyololo, Wilaya ya Mufindi” alisema.
Hata hivyo amesema kuwa, kwa upande wake ataendelea kufanya kazi na vyombo vya habari ikiwemo ushirikiano wa karibu baina yake na wanahabari hao kutokana na umuhimu wao kwa jamii inayowazunguka.
“Kwa upande wangu mimi, nitaendelea kufanya kazi na vyombo vya habari kwa ukaribu kati yangu na waandishi kwa kuwa ni watu muhimu sana kwa jamii inayowazunguka na hasa nikizingatia umuhimu wao katika taifa kwa ujumla” akisema.
Amesema kuwa wanatarajia kufanya mkutano wa hadhara katika eneo la soko kuu la manispaa ya Iringa, ili aweze kuzungumza na wananchi wa manispaa hiyo juu ya masuala mbali mbali yanayojitokeza katika jimbo hilo
.“Hivi karibuni tutafanya mkutano wa hadhara katika eneo la Soko Kuu la Manispaa ya Iringa kuzungumzia masuala mbalimbali yanayojitokeza katika mkoa huu hususani katika jimbo hili lakini ninachowaomba wananchi wasijitokeze katika wiki ya usalama barabarani ikiwa ni moja ya shinikizo la kumuondoa Kamuhanda katika kiti chake” alisema.
![]() |
| Mbunge wa jimbo la Irina Mjini Mch. Peter Msigwa akiwasilisha hoja bungeni |

No comments:
Post a Comment