| Walivyomuua Daud Mwangosi |
Ikiwa ni siku moja tu kupita baada ya kuzagaa kwa taarifa za kuhamishwa Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda, siri ya kuhamishwa kwake zavuja.
Taarifa zilizolifikia gazeti hili kutoka ndani ya jeshi hilo zimeeleza kuwa hatua hiyo imekuja baada ya wananchi kutoonesha ushirikiano kiano katika uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama huku waandishi wa habari mkoa wa Iringa wakiendelea na msimamo wa kutoandika habari za jeshi hilo .
Chanzo chetu cha habari hizi kimeeleza kuwa uamuzi huo umetokea ghafla baada ya Waziri wa mambo ya nadani Emmanuel Nchimbi kufika mkoani hapo katika ufunguzi wa wiki ya nenda kwa usalama na kupokelewa na wanafunzi wa shule za msingi pekee.
“Siku aliyofika Waziri Nchimbi alianza kushangaa kuona watu hawana habari kabisa kama kuna wiki ya nenda kwa usalama ambapo kila mtu alikuwa akifanya shughuli zake na kibaya zaidi alipofika kwenye viwanja wa uzinduzi akapokelewa na na wanafunzi wa shule za msingi pekee ambao hata hivyo inaonekana waliletwa kwa shuruti kwa sababu hakukuwa na watu ili walau kukwepa aibu” kilisema chanzo chetu.
Hata hivyo imeelezwa kwamba wananchi wasingekuwa tayari kufika katika viwanja vya tukio kwa kuwa Kamuhanda hajaonesha kuwajibika au kusema chochote juu ya mauaji ya mwandishi.
“Mauaji ya Mwangosi yanatugharimu sana sasa hivi kiutendaji kwa sababu wananchi wamekosa imani kabisa na jeshi letu. Kila unayetaka kuongea naye kwa kweli haoneshi ushirikiano kabisa. Kibaya zaidi hata mitaani tunakoishi hata wapangaji wenzetu wanatuogopa” kilisema chanzo hicho.
Siku moja kabla ya ujio wa Nchimbi kuliwa na uvumi kuwa kumekuwa na jumbe mbalimbali zilizokuwa zikiokotwa katika geti la ofisi za Kamuhanda zikitoa tahadhari kwake juu uwajibikaji wake kwa jamii.
“Kitu kingine ni kwamba, kunapokucha asubuhi, karibu kila siku makaratasi mbalimbali yamekuwa yakiokotwa nje ya geti la ofisi za kamanda Kamuhanda yakiwa yameandikwa kumtaka akae tayari kwa lolote bila kujulikana yameandikwa na nani” kilisema chanzo hicho.
Kikifafanua zaidi juu ya ujumbe huo chanzo hicho kilisema kuwa maandishi mengi yalikuwa yakimlenga kamanda kuwa ndiye atakaye wajibika na lolote litakalotokea kutokana na kichwa chake kuwa kigumu na kuendelea kung’ang’ania kiti chake huku akishindwa kutoa neno lolote juu ya mauaji yaliypfanyika.
“Labda niseme kwa ufupi tu, ujumbe ulioandikwa kwenye makaratasi hayo unamtaka Kamuhanda akae tayari kwa lolote kutokana na kuendelea kukalia kiti wakati wananchi wanataka ajiuzulu. Ujumbe niliouona kwa macho yangu na kuusoma unasema “Kamuhanda usione wananchi tumekaa kimya ukajua ulichomfanyia mwandishi wetu tumekusifu, endelea kukaa kwenye kiti chako kwa amani” wakati ujumbe mwingine unasema “utakuja kuikumbuka Iringa katika maisha yako, endelea kuwatuma vijana wako watumalize sisi wananchi. Kumbuka wanchi wenzetu uliowaua kule ulikotoa na umefika hapa kuendeleza mauaji yako. Tunakutakia mauaji mema ila usije ukashangaa”. Ujumbe ni mwingi ambao nasikia wenzangu wakisimulia. Hatuna la kufanya kwa sababu hatujui kinachopangwa vichwani mwa watu” kilisema chanzo hicho.
Katika hatua nyingine chanzo hicho kimetoboa siri ya gari la kifahari lililotumika kumfikisha askari Pasificus Cleophace Simon anayemtuhumiwa kwa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha Channel Ten na mwenyeki wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Iringa (IPC) Daud Mwangosi kuwa ni la RCO lililokuwa la RPC zamani.
“Lile gari la kifahari unalolizungumza lilikuwa la RPC zamani kabla ya kununua lingine ambalo analitumia sasa. Lile gari kwa sasa linatumika na RCO N.R. Wankyo – SSP najua kwa majina hayo tu kwa sababu bado ni mgeni hatujayajua majina yake vizuri ili tunapenda kutumua RCO Wankyo hayo ya nyuma hatujayajua” kilisema chanzo hicho.
Kabla ya chanzo hicho kuthibitisha ukweli huo, Tanzania Daima limebaini gari hilo jumapili likiwa limeegeshwa nje ya hotel ya MR likiwa na namba tofauti na zile zilizosomeka siku alipofikishwa mtuhumiwa wa mauaji ya mwandishi yupo mahakamani mwenye namba G2573.
Gari hilo ambalo lilifika mahakamani likiwa na namba za usajili T 320 ACR lilikutwa jumapili likiwa limeegeshwa nje ya hoteli ya MR likiwa na namba T 999 ATC huku kukiwa na watu wengi wanaoaminika kuwa ni askari waliokuwa wamevaa kiraia wakiwa wamezagaa maeneo hayo.
No comments:
Post a Comment