masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Thursday, August 9, 2012

Uvivu wa kufikiri na uzembe wa viongozi ni chanzo cha matatizo nchini

Tanzania ni nchi yenye kila aina ya rasilimali ambazo kama zingetumika kwa ufasahaa zingeeta maendeleo makubwa kwa manufaa ya watu wote.

Licha ya kuwa kumekuwa kukitokea mgao wa umeme unaosemekana kusababishwa na kupungua kwa maji katika mabwawa yanayozalisha umeme nchini, kuna maporomoko ya maji ambayo hayatumiki.

Maporomoko hayo hayahitaji kuongezeka au kupungua kwa maji kwa kuwa maji yanapatikana siku zote 366.

Uvivu wa kufikiri na uwajibikaji duni wa viongozi wetu ni miongoni mwa vikwazo vinavyosababisha kukwama kwa maendeleo hususani kwa upande wa nishati hapa nchini.

Katika milima ya Udzungwa kuna maporomoko ya maji ambayo yangetumika katika kuzalisha umeme tatizo la umeme lingekwisha lakini kwa sababu uvivu wa kufikiri unaandama vichwa vya watu, maji hayo yatabaki katika milima hiyo hadi Mungu mwenyewe aliyeyaumba atakapoamua.

Kama TANESCO wangekuwa na akili ya kuzalisha, wasingetegemea mashine za PTL na majenereta au mashine za umeme wa dharula badala yake wangeweza kuzalisha umeme wa kutosha na wa uhakika kupitia nguvu ya maji hususani katika maporomoko ya milima hiyo.

Mtandao huu gustavchahe.blogspot.com uliweza kutembelea baadhi ya milima hiyo katika kijiji cha Kiwalamo, Itonya, Mhanga na Uluti na kujionea jinsi wenye dhamana hawawezi kufikiri badala yake wanafanya kazi za ubadhilifu wa fedha za umma na kufanya udanganyifu wa badala ya kuwa wabunifu.

Viongozi waliopewa dhamana na wananchi wamekuwa wakikaa kwenye viti vya kuzunguka huku wakipulizwa na viyoyozi na kutumia pesa za walipa kodi bila kuwajibika na kuwatelekeza pasipo kuwapa huduma.

Kwa mfano vijiji hivyo wananchi hawamjui kiongozi yo yote wa serikali kwa kile walichosema viongozi wa kiroho ndio wanaowajibika kuliko wanaotumia kodi zao kwa ajili ya kuwatumikia.

Vijiji hivyo vipo katika Wilaya ya Kilolo ambayo Mbunge mwenye dhamana ni Prof. Peter Msolla ambaye inadaiwa hajawahi kuonekana kwa wananchi hao. Hali kadhalika Mkuu wa Wilaya hiyo pamoja na Mkuu wa Mkoa hawawajui hata kwa majina huku wakipelekewa kofia na viremba vya CCM wavae.

Licha ya kutowajua viongozi hao, hata Diwani huwa haonekani walau kuwasikiliza wananchi shida zao.

No comments:

Post a Comment