masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Tuesday, August 7, 2012

Askofu alaani waharibifu wa miundombinu
































Waharibifu wa miundombinu wamelaaniwa vikali kuacha tabia hiyo kwani ni moja ya sababu inayorudisha maendeleo nyuma.

Hayo yamezungumzwa jana na Rais wa Baraza la maaskofu Tanzania ambaye pia ni askofu wa jimbo la Iringa Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa katika sherehe za Kipaimara zilizofanyika katika Kanisa la Mt. Teresia wa Mtoto Yesu Parokia ya Madege jimboni humo.

Amesema kuna watu ambao kwa makusudi wanaamua kukwamisha shughuli kwa kuharibu miundombinu ambayo ingeleta faida katika mazingira wanayoishi wenyewe.

Katika mradi wa umeme anaouendesha katika Maguta parokiani humo Mhashamu askofu Ngalalekumtwa amesema inashangaza na inasikitisha mtu anaojitolea kufanya jambo kwa faidi ya jamii, baadhi ya watu wanafanya jitihada za kukatisha tamaa ili shughuli isiendelee.

“Leo naomba niwaambie ukweli bila kuficha, ule mradi wa umeme unaofanyika pale Maguta ni wa kwangu na lengo langu siyo kupeleka mjini kama mnavyodhani, huo utabaki kuwa mali yenu kwa kuwa umeme utasambazwa majumbani mwenu; nitahakikisha umeme wa kutosha umesambaa katika nyumba zenu ndipo nitakapo amua kuwapelekea wengine” alisema.

Katika ujenzi wa mradi huo kumekuwa kukiripotiwa kutokea hujuma za vifaa na mambo mengi ambayo yanakatisha tamaa jambo ambalo amekemea na kulaani vikali.

“Nina laani vitendo mbalimbali vinavyofanywa na baadhi ya watu kukatisha tamaa kutoendelea mbele kwa mradi huo, mimi ni mtu mzima siwezi kudanganyika, nina uelewa wa kutosha. Nimeamua kujenga mradi huo kwa manufaa yenu kwa kuwa kama ni umeme kwangu upo, huo unaotengenezwa ni kwa manufaa yenu lakini kumekuwa na baadhi ya watu wanafanya hujuma na jitihada za kila aina ya vikwazo ili tu kukwamisha kazi hiyo isiendelee mbele; nina laani kwa masikitiko makubwa, vilaaniwe vitendo hivyo na si hapa tu nchini kote kwa wale wote wanao haribu miundombinu laana iwe juu yao kwa kuwa wanakwamisha maendeleo ya wengi” alisema.

Mradi huo unamilikiwa na jimbo Katoliki la Iringa ambapo kufikia desemba mwaka huu vijiji vitatu: Madege, Ilutila na Idete vinatarajiwa kunufaika na umeme.

Katika sherehe hizo jumla ya vijana 186 walipewa Sakramenti ya Kipaimara wakitanguliwa na 56 waliopewa katika Kanisa la Mwenyeheri Yosefu Allamano kigango cha Kiwalamo pamoja na 42 waliopewa katika kigango cha Itonya na kufikisha jumla ya vijana 284 waliopewa Kipaimara huku Mhashamu askofu Ngalalekumtwa akibariki Kanisa la Kigango cha Mhanga ndani ya Parokia hiyo.

No comments:

Post a Comment