| Huo ni muonekano wa soko la Kalenga jimbo la Mbunge William Mgimwa (Waziri wa fedha nchini) |
| Mmiliki wa mtandao huu Gustav Chahe akiulizia bei katika soko la Kalenga |
| Mmiliki wa mtandao huu akisikiliza maelezo ya mfanyabiashara wa soko hilo. |
| Bidha mbalimbali za vyakula zikiwa sokoni. |
| Hii ni sura ya soko la Kalenga. |
| Hili ni jengo la soko la Kalenga lililotelekezwa kabla halijaisha na sasa linabomoka. |
Ukitamka Wizara ya fedha katika nchi ya Tanzania hutakuwa umemaliza bila kumtaja William Mgimwa mwenye dhamana.
Hali kadhalika ukimtaya waziri huyo unakuwa na maana ya Mbunge wa jimbo la Kalenga lililopo katika mkoa wa Iringa.
Kalenga ni moja ya sehemu ya utalii katika nchi ya Tanzania ambako fuvu la kichwa cha Mtwa Mkwawa Chifu wa wahehe limehifadhiwa.
Wageni mbalimbali hufika katika makumbusho hayo kuona fuvu hilo kwa manufaa ya taifa.
Licha ya kufikiwa na wageni mbalimbali katika eneo hilo, soko halipo pamoja na kuwepo wafanyabiashara mbalimbali.
Jengo ambalo lilikuwa likijengwa kama soko nalo lilitelekezwa na hatimaye sasa linaanguka.
Katika hali isiyo ya kawaida haiingii akilini kuona vibanda ambavyo wafanyabiashara wanavitumia kama soko huku wakiendelea kulipa ushuru ambao huitw uhushuru wa soko.
Je, Waziri wa fedha ambaye ni Mbunge wa jimbo hilo ana mchango gani kwa wafanyabiashara na kwa raia wote kwa ujumla wa maeneo hayo?
No comments:
Post a Comment