masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Monday, July 30, 2012

Watanzania wanataka kujua aliyemtesa Dkt. Ulimboka

Mwenyekiti wa BAVICHAJohn Heche nyuma yake Katibu wa BAVICHA taifa wakiwasili katika kiwanja cha Mbwembetogwa kwa ajili ya kuwa ajili ya kuwahutubia wakazi wa Iringa

Mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa wa Njombe Lulandala Raphael akiwahutubia wakazi wa Iringa

Katibu mstaafu wa CHADEMA Mkoa wa Iringa Pascal Bella akiwahutubia wakazi wa Iringa

Katibu wa BAVICHA taifa Deogratius Munishi akiwahutubia wakazi wa Iringa

Mwenyekiti wa BAVICHA taifa John Heche akiwahutubia wakazi wa Iringa katika kiwanja cha Mwembetogwa

Wakazi wa Iringa wakimsikiliza mwenyekiti wa BAVICHA taifa

Mwenyekiti wa baraza la vijana Chadema Taifa (BAVICHA) akiwahutubia wakazi wa Iringakwenye uwanja waMwembetogwa.



Jeshi la Polisi nchini limetakiwa kumhoji Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Kayanza Pinda kuhusiana na unyama aliofanyiwa kiongozi wa chama cha madaktari nchini Steven Ulimboka huku Watanzania wakitaka kujua aliyemfanyia unyama huo.

Haya yamezungumzwa na Mwenyekiti wa baraza la vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kitaifa BAVICHA John Heche katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika viwanja vya Mwembetogwa ndani ya Manispaa ya Iringa.

Alisema inasikitisha kuona mpaka leo hakuna Polisi hata mmoja aliyemhoji Pinda juu ya kuteswa kwa Dkt. Ulimboka kwa kile alichosema “liwalo na liwe”.

“Ninashangaa kuona mpaka leo hakuna polisi aliyemhoji Pinda juu ya unyama aliofanyiwa Dkt. Ulimboka; hii inaonesha jinsi nchi ilivyokosa usalama au inaonesha ni jinsi tukio hilo lilivyotengenezwa kwa ajili ya maslahi ya watu wachache” alisema Heche.

Pamoja na kuhojiwa Pinda, alisema watanzania bado wana hamu  kubwa ya kumjua aliyefanya unyama huo ili kuona haki ikitendeka kwa kila mmoja vinginevyo watakosa imani kwa vyombo vya usalama.

“Watanzania bado wana hamu kubwa ya kumjua aliyemfanyia unyama daktari huyo ili kuona haki ikitendeka vinginevyo watakosa imani kwa vyombo vya usalama hapa nchini” alisema.

Kutokana na tukio hilo amesema linatokana na udhaifu wa Rais Kikwete, Pinda na Spika wa Bunge Anne Makinda kwa kushindwa kumaliza kiu ya watanzania kwa kuyaweka wazi masuala yanayoihusu jamii.

“Haya yote yanatokana na udhaifu wa Kikwete, Pinda na Spika wa Bunge Anne Makinda kwa kushindwa kuyaweka wazi masuala yanayoihusu jamii kama la kuteswa kwa daktari huyo” alisema.

Alisema inashangaza kuona mawaziri wanaongozana kama makondoo kwenda huku na huko kuwahutubia watu juu ya umoja na amani huku wakiendelea kukaa kimya juu ya aliyemtesa Ulimboka.

“Inashangaza sana kuona mawaziri wanaongozana kama makondoo huku na huko wakiwahutubia watu juu ya umoja na amani huku wakishindwa kuwaeleza watanzania juu ya aliyemtesa Ulimboka; ni umoja gani wanaouzungumzia watu hao, ni amani gani wanayoizungumzia watu hao wakati unyama unafanyika bila kuchukuliwa hatua yoyote? Huu ni udanganyifu mkubwa” alisema Heche na kuhoji.

Amewataka watanzania kutokubali propaganda za CCM zinazowagawa katika makundi ya kidini kwani huo ni uhuni unaohatarisha usalama wa raia.

“Msikubali propaganda za CCM zenye malengo ya kuwagawa kidini kwani wamekosa sera na kuanza kutumia dini kama kinga yao. Chadema siyo chama cha kidini kama wanavyosema CCM. Kumbuka walipoona Chama cha Wanchi CUF kina nguvu wakasema ni cha kiislamu wakafanikiwa kukiua ili wao waendelee kuwa madarakani kuwanyonya na kuwatesa watanzania. Leo hii wameona Chadema ina nguvu wameanza propaganda zile zile za udini. Wapuuzeni na msikubali kubadilisha mawazo yenu. Kama CUF nkilikuwa chama cha Kiislamu na sasa wanasema Chadema ni cha Kikristo, je, wao CCM ni cha dini gani? Msisikilize propaganda zao piganieni haki zenu hadi kieleweke” alisema.

Naye katibu wa BAVICHA taifa Deogratius Munishi alisema CCM na Serikali yake inaendesha mauji ya raia wake wasio na hatia ili tu wasiwe na sauti ya kuhoji na kudai haki wanazonyimwa na chama hicho.

“CCM na serikali yake inaendesha mauji ya raia wake nchini ili wasipate nafasi ya kuhoji na kudai haki zao wanazonyimwa; wanachukua vijana na kuwapeleka kwenye makambi kwa ajili ya kuwafundisha namna ya kudhulu watanzania wanaodai na kuhoji haki zao” alisema Munishi.

Amesema ni kitu cha aibu kuona serikali inatumia nguvu badala ya kutekeleza majukumu yake kwa raia.

“Ni kitu cha aibu sana kuona serikali inatumia nguvu kwa kuwaua raia badala ya kutekeleza majukumu yake; serikali imefubaa kimawazo, kiakili na ina utapiamlo wa kimawazo” alisema.

Amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi kutoa maoni ya mabadiliko ya Katiba itakayowawezesha kuwa na sauti ya kulinda haki zao.

“Jitokezeni kwa wingi kutoa maoni juu ya mabadiliko ya Katiba kwani hiyo ndiyo njia pekee ya kulinda haki zenu na kuwa na sauti ya kuhoji juu ya haki mnazonyimwa” alisema.

Katika mkutano huo jumla ya watu 201 walichukua kadi za CHADEMA.

No comments:

Post a Comment