masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Saturday, August 11, 2012

Askofu: Mali za wizi siyo za kutolea shukrani kwa Mungu


Wanaojiona kuwa mali zao ni za wizi walizipata kwa njia isiyo halali wametakiwa kutokupeleka Kanisani kama njia ya kumshukuru Mungu kwa kuwa ni laana kubwa katika kumjaribu Mungu.

Hayo yamesemwa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Iringa Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa wakati wa maadhimisho ya Misa ya Shukrani kwa Mungu iliyofanyika jana katika Kanisa Kuu la Kiaskofu la Moyo Mt. wa Yesu Parokia ya Kihesa jimboni humo.

“Kama unajiona kuwa mali zako au kipato chako ni cha wizi au unapata kwa njia isiyo halali, usije kumshukuru Mungu hapa mbele kwa sababu ni laana; Mungu hapendi udanganyifu bali anataka kila kitu kitendeke kwa haki ili kila mtu aridhike” amesema askofu Ngalalekumtwa.

Askofu Ngalalekumtwa ambaye pia ni Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, amesema mtu ye yote mwenye moyo wa shukrani ni muungwana kwa kuwa huthamini kile alichopewa hata kama ni kidogo.

“Ukiwa ni moyo wa shukrani ni uungwana kwa kuwa unathamini kile unachokipokea hata kama ni kidogo lakini ukiwa na moyo wa ubinafsi ni udhurumaji kwa kuwa hupenda kujilimbikizia mali hata isiyo halali” amesema.

Amesema baadhi ya watu wamekuwa wakidhani kuwa kila kitu ni ali yao na kuwanyanyasa wengine wasio na kitu bila kutambua kuwa wamejaliwa na Mungu na wanapaswa kumrudishia shukrani.

“Kuna watu ambao huamini kuwa kila kitu walicho na cho ni mali yao na kutumia nafasi hiyo kwa kuwanyanyasa wengine wasio na kitu bila kujua kuwa kilie walichonacho wamejaliwa na Mungu na wanapasika kumrudishia shukrani kwa kufanya matendo ya huruma” amesema.

Maadhimisho ya siku hiyo zaidi ya shilingi milioni 48 zilikusanywa kama shukrani kwa Mungu kwa ajili ya kusaidia kazi mbalimbali za uinjilishaji katika ofisi za askofu ikiwa ni pamoja na matendo.

No comments:

Post a Comment