| Fill Karashani akitoa maelezo kwa waandishi wa habari katika ukumbi wa Maktaba ya Mkoa wa Iringa |
Mwaandishi wa habari za makala mzuri anatakiwa kuwa na kipaji cha kuandika habari hizo japokuwa elimu inahitajika katika kujua sheria na kanuni zake.
Kauli hiyo imetolewa leo na Fill Karashani wakati akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Iringa yanayoendelea kufanyika katika ukumbi wa maktaba ya mkoa.
Karashani alisema ili mwandishi wa habari za makala awe mzuri na makini ni lazima awe na kipaji katika kuandika habari za makala ili kusaidia jamii kuelezea matukio mbalimbali yanayotokea ndani na nje ya nchi.
Katika kutayarisha makala makala nzuri yenye manufaa kwa jamii, mwandishi ametakiwa kutumia muda mzuri katika kufanya upembuzi yakinifu ili kukabiliana na changamoto zinazoweza kutokana na tukio analoliandika.
Alisema ni wajibu wa mwandishi wa makala kutumia kipaji chake na taaluma katika kuisaidia jamii kwa hali yoyote ili kujua mambo yanayoilenga kwa ajili ya ufanisi katika maisha ya kila siku.
Naye Katibu wa chama cha waandisdhi wa habari katika mkoa wa Iringa Frank Leonard amewatka waandishi kujikita katika uandishi wa makala ambao huchimbua habari kwa undani ili kuifikishia jamii ujumbe stahiki kwa uazi zaidi.
“Ni vema waandishi kufanya mabadiliko ya uandishi na kujikita katika uandishi wa makala ili kuiwezesha jamii kupata habari inayoeleweka kwa undani ili kurahisisha uelewa wa jambo au tukio husika” alisema.
Frank pia alishukuru SIDA kupitia UTPC kufadhili mafunzo hayo ambayo ni mahsusi kwa ajili ya kuendeleza taaluma na ujuzi wa waandishi wa habari katika kuandika makala.
Mafunzo ya uandishi wa makala ni ya siku nne yakitanguliwa na mafunzo ya uandishi wa habari za uchunguzi yaliyofanyika wiki moja iliyopita.
No comments:
Post a Comment