masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Tuesday, August 28, 2012

Mkutano wa CHADEMA wasitishwa Iringa > Polisi wapiga marufuku > Wadai kupisha zoezi la sensa

Mbunge wa viti maalum (CHADEMA) Chiku Abwao akiwatangazia wananchi kuahirishwa kwa mkutano leo

Abwao akiongea na kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Michael Kamhanda juu ya kuahirishwa kwa mkutano


Mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA uliotarajiwa kufanyika masaa machache yaliyopita katika viwanja vya Mwembetogwa mjini Iringa umesitishwa na jeshi la polisi.

Mkutano huo umesitishwa ikiwa ni sikumoja tu baada ya jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa kutoa kibali cha kufanyika huku wakitaka wahusika wa mkutano huo sehemu moja ya kufanyia kati ya Mbembetogwa na Mlandege.

Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu ofisini kwake Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Michael Kamhanda amesema jeshi hilo limeamua kusitisha mkutano huo kwa sababu ya sensa kuendelea, kutokana na maafa yaliyotokea Morogoro katika maandamano pamoja utafiti wa kiintelijensia.

"Tumesitisha mkutano huo kwa sababu tatu: moja kupisha sensa inayoendelea kufanyika kwa uhuru, pili ni kutokana na vurugu zilizotokea huko Morogoro na kusababisha maafa na tatu ni kutokana na sababu za kiintelijensia ambazo tumebaini kuwa kunaweza kutokea uvunjifu wa amani" alisema Kamhanda.

Polisi wameamua kufanya doria siku nzima kupitia kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) huku wakiwa na silaha za moto kuzunguka maeneo yote ya Manispaa kuhakikisha kuwa hakuna mkutano wa CHADEMA unaofanyika sehemu yo yote hadi hapo zoezi la sensa litakapopita.

Moja ya gari lililotumika katika doria hiyo lina namba za usajili PT 1404 ambalo lilionekena katika ofisi za CHADEMA Wilaya ya Iringa majira ya saa 5 asubuhi.

Magari mengi ya polisi yalionekana kuzunguka mji mzima hali iliyosababisha wananchi kuwa na hofu juu ya usalama wao kwa kuwa si kawaida kufanya doria ya aina hiyo na hata pale wanapohitaji polisi mahala fulani polisi wamekuwa wazito kufika kwa wakati.
 
Jeshi la polisi lilitoa kibali kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo jana kukubali kufanyika mkutano huo ambao ghafla leo jeshi hilo limeamua kupiga marufuku.

Barua ya jeshi la polisi kuruhusu mkutano huo ina kumbukumbu namba namba IRI/A.24/9/VOL/180 ambayo ilisainiwa na Mkuu wa polisi wa wilaya ya Iringa, ikiwa na kichwa cha habari kinachotoa toa ruhusa ya kufanyika kwa mkutano na maandamano.

Akiahirisha mikutano huo mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chadema Mkoani Iringa, Chiku Abwao alisema wameamua kukubali matakwa ya polisi ili kuepusha uvunjivu wa amani unaoweza kutokea.

Abwao amewataka wafuasi wa chama hicho kuwa watulivu wakati huu ambao wamezuiwa kufanya mikutano yoyote hadi pale watakapokubaliwa baada ya kuisha kwa zoezi la sensa ya watu na makazi.

No comments:

Post a Comment