masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Thursday, August 23, 2012

Watanzania washauriwa kupokea Teknolojia mpya

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Christine Ishengoma akifungua warsha ya mawasiliano katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria Iringa



Mshiriki wa warsha akipotea zawadi baada ya kujibu swali


Washiriki wa warsha wakiwa katika picha ya pamoja
Ishengoma akifunga warsha


Watanzania wametakiwa kuwa tayari kupokea mabadiliko ya kiteknolojia ifikapo desemba mwaka huu ambayo inaweza kuathili baadhi ya mawasiliano.

Haya yamezungumzwa na Mkurugenzi wa tume ya mawasilinao Tanzania Addy Mkunze katika warsha ya siku moja iliyofanyika kwa wadau wa habari mkoa wa Iringa katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria.

Tangu kuanza utangazaji Mosi Julai, 1951, Tanzania ilikuwa ikirusha matangazo hayo kwa njia ya analojia ambayo inaonekana kutokuwa na ubora wa matangazo hata wakati mwingine mawasiliano kuingiliana mara kwa mara.

Kutoka katika analojia mawasiliano yanahama kwenda dijitali ili kurahisisha usikivu na upatikanaji wa huduma zenye ubora kwa kuzingatia umuhimu wa mawasiliano duniani ambapo televisheni pekee ndizo zitakazoingia katika mabadiliko hayo huku redio zikiendelea na matangazo kama kawaida hadi hapo muda utakapofikia kuingia katika mabadiliko.

Imeelezwa kawa redio zitaendelea na matangazo kwa kuwa ni chombo muhimu sana ambacho kinamgusa hata mtu wa hali ya chini licha ya kuwa utafiti unaendelea kwa ajili ya mabadiliko.

“Redio hazitahusika na mabadiliko hayo kwa sababu ni chombo muhimu sana ambacho kinamgusa hata mtu wa hali ya chini pamoja na kuwa utafiti unaendelea kwa ajili ya mabadiliko” alisema.

Licha ya kuwepo aina tatu za utangazaji yaani utangazajia wa mitambo kusimikwa ardhini, Kebo na Satelaiti, utangazaji kwa njia ya satelaiti utaendelea kuwepo.

Utangazaji wa kidijitali unakusudia kupunguza matumizi ya nishati kwani mitambo yake hutumia nishati ya umeme ndogo, kutumia muda mchache kutayarisha kipindi, kuwa na ubora wa sauti na picha, kuwa na vifaa vichache vya kuhifadhia habari nyingi na vipindi ikiwa ni pamoja na kuwa na maktaba ndogo ya kuhifadhi vipindi kulinganisha na vifaa vya analojia.

Pamoja na faida hizo, watanzania wametakiwa kuwa makini na wasambazaji wa vifaa vya mawasiliano hayo ili kuepuka kununua vifaa visivyo na ubora ikiwa ni pamoja na kuhakikisha vifaa vinavyouzwa vinakuwa na garantii ya muda mrefu.

Tanzania ni miongoni mwa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo inatekeleza mpango wa kuboresha mawasiliano kutoka analojia kwenda dijitali ifikapo Desemba 31, 2012 ambapo mitambo ya analojia itazimwa.

Tanzania imeingia katika mfumo wa utangazaji wa Dijitali badala ya Analojia baada ya kutungwa kwa sheria mpya ya mawasiliano (EPOCA 2010) ili kutumia kikamilifu masafa ya utangazaji na kuongeza ufanisi wa vituo vya utangazaji ambayo imeupa nguvu kisheria mkakati mzima wa uhamaji kutoka mfumo wa utangazaji wa Analojia kwenda Dijitali.

No comments:

Post a Comment