| Thomas Zacharia mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCO) akiwahutubia wananchi wa Ulonge |
| Baadhi ya wananchi wa Ulonge wakisikiliza wanafunzi wa vyuo vikuu |
| Joseph Mtama mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mkwawa akiwahutubia wananchi wa Ulonge |
| Frank Malata mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ruaha akiwahutubia wananchi wa Ulonge |
| Frank Mwankina mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ruaha akiwahutubia wananchi wa Ulonge |
| Jesca Kishoa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Rauaha akiwahutubia wananchi wa Ulonge |
| George Tito mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mkwawa akiwahutubia wananchi wa Ulonge |
| Nicolaus Mpandula mwanafunzi wa RUCO akiwahutubia wananchi wa Ulonge |
| Mkanyia Timotheo akiwahutubia wananchi wa Ulonge |
| Rose Mayemba mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ruaha akiwahutubia wananchi wa Ulonge |
| Jesca Kishoa mwanafunzi wa RUCO na George Tito mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mkwawa wakijianda kuanza mkutano. |
Wananchi wameshauriwa kuhoji viongozi wao juu ya michango wanayochangia kwa ajili ya maendeleo ili kujua matumizi yanakwendaje.
Haya yamezungumzwa na wanafunzi wa vyuo vikuu vya mkoani Iringa jana walipokuwa wakitoa elimu ya uraia kwa wananchi wa kijiji cha Ulonge lilichopo mpakani kwa Manispaa na Wilaya ya Kilolo.
Wamesema ni haki ya wananchi kujua michango yao inatumika kwa kazi gani na kuchukua hatua pale wanapoona kuna udanganyifu katika matumizi hayo.
Wamesema wapo baadhi ya viongozi wanaowachangisha michango wananchi kwa ajili ya masuala yao binafsi na kutoa taarifa za uongo ili kumridhisha mwananchi huku wakijua kuwa ni uongo.
Sambamba na hilo wamewataka wananchi washiriki katika mchakato wa katiba mpya ili kutoa mawazo yao kwa ajili ya maendeleo ya taifa.
Wamesema Taifa lolote linamtegemea kila mtu na mchango wake kwa ajili ya maendeleo na hivyo wao wananchngo mkubwa katika mabadiliko ya katiba.
Vyuo vikuu vilivyopo katika mkoa wa Iringa ni Chuo Kikuu cha Tumaini, Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCO) na Chuo Kikuu cha Mkwawa.
No comments:
Post a Comment