| Msikwa Victor mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ruaha akihutubia wananchi katika viwanja vya Igumbilo |
| Mwanawima Salezi mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ruaha akiwahutubia wanchi |
| Malata Frank mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ruaha akiwahutubia wananchi |
| Jesca Kishoa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ruaha akiwahutubia wananchi |
| Msangi Augustino mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ruaha akiwahutubia wananchi |
| Mwankina Frank akiwahutubia wananchi katika viwanja vya Igumbilo |
| Mpandule Nicolaus akiwahutubia wananchi katika katika viwanja vya Igumbilo |
| Nuru ramadhani akiwahutubia wananchi katika viwanja vya Igumbilo |
| Oscar Sanga mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ruaha akiwahutubia wananchi |
| Mkanyia Timotheo akiwahutubia wananchi katika viwanja vya Igumbilo |
| Sikanla Luka mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ruaha akiwahutubia wananchi |
| Rais wa Chuo Kikuu kishiriki cha Mkwawa Mtama Joseph akiwahutubia wananchi wa Igumbilo |
| Masifia Sunda akiwahutubia wananchi wa Igumbilo |
| George Tito mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mkwawa akiwahutubia wananchi wa Igumbilo |
Suala la mchakato wa katiba mpya linaonekana bado ni kitendawili kwa wananchi kutokana na kutoijua wala kuiona katiba iliyopo na kubaki masimulizi kwao.
Wananchi wa kata ya Ruaha katika Manispaa ya Iringa wamesema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanywa na wanafunzi wa vyuo vikuu vya mkoa wa Iringa uliofanyika jana katika viwanjwa vya Igumbilo.
Wananchi hao wameomba kuelimishwa juu ya katiba inayotumika kwa sasa ili kujua ni wapi wangekuwa na sauti ya kutolea maoni yao juu ya uundwaji wa katiba mpya.
Wakizungumza katika mkutano huo wanafunzi hao wamesema kuwa kutokujulikana kwa katiba kwa wananchi kunatokana na mfumo mbovu wa uongozi wa chama tawala ambao kwa makusudi wamewanyika wananchi katiba ili wasijue haki zao kusudi wanyonywe vizuri.
Wamesema kuwa kutoiweka wazi katiba ya taifa kunasababishwa na watu wachache wanajilimbikizia mali na kuwanyang’anya wananchi ardhi zao na kuwapatia wageni.
“Wananchi wa Tanzania hawapewi nafasi katika kumilikishwa ardhi na badala yake wananyang’anywa hata sehemu kidogo walizokuwanazo na kuwapatia wageni; huu ni utaratibu mchafu wa serikali ya chama cha mapinduzi CCM iliyojaa rushwa, ubabaishaji, udanganyifu na uhuni wa kila aina kwa kuwanyima katiba wananchi” alisema Msokwa Victor.
Naye Rais wa chuo Kiku cha Mkwawa Mtama Joseph akihutubia katika mkutano huo alisema kuwa nchi ya Tanzania inazidi kutia aibu ya kuomba licha ya kuwa na rasilimali nyingi za kila aina.
“Ni aibu kubwa kwa Taifa kama hili lenye rasilimali nyingi za kila aina kuongoza kutembeza bakuli na kuombea misaada kwa miaka 50 ya uhuru. Huu ni upuuzi, huu ni udharirishaji, huu ni uhuni wa hali ya juu” alisema Mtama.
Wanafunzi wa vyuo vikuu vya mkoani humo waliohutubia ni Msokwa Victor, Mwanawima Salezi, Malata Frank, Nuhu Ramadhani, Oscar Sanga, Mkanyia Timotheo, Sinkala Luka, Mtama Joseph, Masifia Sunda na George Tito.
Vyuo vikuu vya mjini Iringa ni pamoja na Chuo Kikuu cha Mkwawa, Chuo Kikuu cha Tumaini pamoja na Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCO).
No comments:
Post a Comment