masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Tuesday, July 17, 2012

Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Kilolo ajiuzulu > Pesa za CCM zamponza > Adaiwa kuwa kibaraka wa kigogo mmoja wa CCM

Wajumbe wa kikao cha chama wakimsikiliza hoja

Clay Mwitula akitoa maelezo alipokuwa akijiuzulu

Olian Mkemwa mwenyekiti wa muda akiwa kwenye kiti cha uenyekiti baada ya aliwekuwa mwenyekiti kuchomoka


Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA katika Wilaya ya Kilolo Clay Mwitula amejiuzulu wadhifa huo katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa SUN uliopo Ilula katika Wilaya hiyo.

Kikao kilichofanyika Juni 14, mwaka huu kililenga kujadili uchaguzi unaotarajiwa kufanyika ndani ya chama hicho katika ngazi ya mashina hadi kamati kuu.

Katika mjadala uliodumu kwa muda wa takrinani masaa 4 wajumbe wa mkutano huo walisema hawawezi kujadili juu ya uchaguzi kama mwenyekiti huyo hawezi kuachia nafasi yake kwa kile walichosema ameshindwa kuwajibika katika nafasi yake kama mwenyekiti na kutoa taarifa za uongo juu ya utendaji wake.

Tuhuma nyingine aliyotakiwa kuwajibika ilionekana mwenyekiti huyo anaingilia nafasi za watu wengine huku wenye nafasi wakiwapo bila kushirikishwa ikiwa ni pamoja na kutokuitisha mikutano na vikao kwa mujibu wa katiba ya chama.

Katika mvutano huo Mwitula alionesha kutokukubali kuwajibika na kusababisha wajumbe kupandwa na jazba wakitaka kung’oa kwa nguvu jambo ambalo liliingiliwa na katibu mwenezi wa Wilaya hiyo Cosmas Mmehwa na kuwataka wajumbe watulie kumpa nafasi mwenyekiti huyo aweze kutafakari na kutoa maamuzi sahihi ushauri uliozaa matunda mazuri.

Awali ilidaiwa kuwa mwenyekiti huyo amekuwa hana mawasiliano mazuri na viongozi wenzake ikiwa ni pamoja na kutumia kiti chake vibaya na kuwakera wananchama pale walipokuwa wakihitaji maelekezo ya chama.

Licha ya kushinikizwa na baadhi ya wanachama kuomba msamaha kwa nguvu, msamaha wake haukupokelewa na kwa kile walichomtaka kujivusa wadhifa huo kwa kuwa hata angepewa msamaha wamachama wamekosa imani naye.

Mwitula anazungumzwa kuwa anatumiwa na Mbunge wa jimbo la Kilolo Profesa Peter Msolla kwa mfuko maalumu ili kukidhoofisha CHADEMA katika Jimbo hilo kwa kile kilichoelezwa na wanachama kuwa hata wakati wa operesheni sangara alipewa pesa na mbunge huyo akatoa taarifa za uongo kuwa kuna mvua wakati ilikuwa ni kiangazi ili mradi tu mikutano hiyo isifanyike ndani ya jimbo hilo tuhuma ambazo Mwitula amezikanusha mbele ya mkutano huo.

Olian Mkemwa ndiye aliyekalia kiti hicho kwa muda mpaka hapo utaratibu wa kumpata mwenyekiti utakapofanyika.

Hii ni mara ya kwanza katika Wilaya hiyo wanachama wa chama hicho kukosa imani na kiongozi wa ngazi ya Wilaya na wananchama kuahidi kuwa endapo kiongozi ye yote atapoteza sifa hatafumbiwa macho kwa kuwa CHADEMA ni chama pekee kisicholinda ubovu wowote kwa mwanachama ye yote.

Kikao hicho kilihudhuriwa na jumla ya wajumbe 38 mahudhurio yaliyokidhi vigezo vya kufanyika kwa kikao hicho kwa mujibu wa katiba ya chama hicho.

No comments:

Post a Comment