| Hii ni barabara inayotoka Tumaini kuelekea Gangilonga ikiwa imetengenezwa kwa kiwango cha changarawe. Ni miaka mingi haijawahi kutengenezwa |
Kabla watanzania walioowengi hawajaelevuka viongozi mbalimbali walitumia njia mbalimbali katika kuwadanganya ili wapigiwe makofi.
Tanzania ya leo si ile ya mwaka 1977. Miaka ya nyuma unapoaongea jambo ilikuwa haijalishi una ushahidi au huna kwa sababu hakukuwa na mtu anayeweza kuomba ushahidi na kama walikuwepo ikionekana huna ilikuwa ikujulikana ni uongo tu lakini siku za leo unapoongea jambo lazima uwe umejizatiti kwa ushahidi wa kutosha.
Willibroad Slaa alipokuwa bungeni wakati analipua upotevu wa pesa za benki kuu au BoT na EPA alionekana kama mwendawazimu. Kadiri siku zilivyokuwa zikisogea ukweli ulionekana nana watu wakaanza kuishi kwa mashaka.
Nani asiyejua suala la BoT na EPA leo hii? Hata mtoto wa darasa la tatu analijua.
Mtoto anapolia anaweza kubembelezwa kwa pipi au ua ili anyamaze. Hii ni nia rahisi sana haihitaji ujuzi au elimu ya juu.
Wakati Iringa mjini ikiongozwa na mbunge wa CCM Mama Monica Mbega, wananchi walikuwa kama watoto wanaobembelezwa kwa pipi au ua.
Watu walipewa mavazi ya CCM hususani akina mama walipewa vitenge kofia na akina baba t-shirt na kofia lakini kwa upande wa mavazi ya chini kwa maana ya suruali au sketi hawakupata. Walitakiwa kusetiri mwili nusu yaani kuanzia kichwani hadi kiunoni tu na kwa habari ya kiunoni hadi nyayoni hiyo ilikuwa ni juu yao.
Naam! Siyo Iringa tu hata sehemu nyingine mpaka leo hususani katika majimbo yanayoongozwa na wabunge wa chama cha mapinduzi CCM.
Nia yangu siyo hiyo bali japo nimeona nidokezee kwa ufupi. Katika Manispaa ya Iringa masuala ya miundombinu ilikuwa kitendawili japo kuwa mbunge huyo alisema anafanya kazi. Walikuwa wakipitisha mashine wakati anapokuja kiongozi Fulani wa kitaifa kwa kuziba mashimo tu au wakati mwenge unapita. Kwa maneno mengine hiyo ni danganya toto.
Wananchi waligeuzwa kama watoto wakudanganywa kwa pipi na kubaki wakipigwa mchanga wa macho.
Leo hii Iringa mjini inaongozwa na Mbunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mch. Peter Msigwa.
Licha ya kuwa anapoanza kazi hakulikuta faili lolote katika ofisi na milango ya ofisi ikiwa imeng’olewa vitasa hadi mapazia, Iringa inaonekana kwa sura nyingine.
Haijalishi alianza katika mazingira magumu lakini anajitahidi kuibadilisha Iringa hata pale ambapo wananchi walikuwa wamesahaulika wanakumbukwa sasa.
Miundombinu inaonekana kuwaridhisha wananchi hasa barabara za mitaani ambazo hazijawahi kuguswa sasa hivi zinaonekana kwa sura mpya.
Ni miaka michache tu imepita taangu aingie madarakani lakini anaonekana kuleta matumaini kwa wananchi. Japo kuwa barabara hizi zinakumbukwa kwa changarawe zinakuwa na uahueni wa kupitika na sasa barabara ya Chuo Cikuu cha Tumaini inajengwa kwa kiwango cha lami
Hata katika hospitali ya mkoa na ya wilaya amejitahidi kuchangia kwa ajili ya kuondosha usumbufu kwa wagonjwa wanaolazwa katika hospitali hizo.
Watanzania wa leo hawadanganyiki kirahisi kwani wamekuwa ni watu wa kuhoji kila kinachofanywa na viongozi wao
Dodoso hizi ni changamoto kwa viongozi wanaojisahau wakipewa nafasi na pia zinabaki kuwa changamoto kwa wananchi kutomuangalia mtu sura wakati wa uchaguzi bali kuangalia uwajibikaji wa mtu katika kazi.
No comments:
Post a Comment