| Maji yakitoka nje ya ukuta wa shule hiyo |
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Iringa (Iringa girls) na wananchi wanaoizunguka shule hiyo wapo hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko.
Magonjwa hayo yanaweza kutoke kutokana na maji machafu yanayotiririka kutoka katika shule hiyo bila kufanyiwa utaratibu wa kuyadhibiti.
| Maji yakiwa yamezagaa nje ya uzio yakitafuta welekeo |
Katika uchunguzi uliofanywa na mtandao huu (gustavchahe.blogspot.com) mapema hii leo umebaini kuwa maji hayo yanatoka katika vyoo vya shule hiyo.
Ni mara kwa mara maji hayo yanajitokeza yakitiririka bila hatua yoyote kuchukuliwa ambapo kwa wakati huu tangu yaanze kutiririka ni zaidi ya wiki moja hayajachuliwa hatua stahiki.
Mmoja wa waalimu katika shule hiyo ambaye ameomba jina lake lisiandikwe amesema suala la maji hayo linajulikana lakini uzembe unatokana na uongozi wa shule hiyo kutokuchukua hatua za haraka.
Juhudi za kumpata mkuu wa shule hiyo zimegonga mwamba kwa kile kilichoelezwa shuleni hapo kuwa siku za jumamosi si rahisi kwa mkuu huyo kuonekana shuleni hapo.
No comments:
Post a Comment