masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Tuesday, July 24, 2012

Watatu wafa na wengine 17 kujeruhiwa vibaya katika ajali mlima Kitonga

Basi likiwa limelala barabarani baada ya kuanguka


Na Gustav Chahe, Iringa

Watu watatu wamekufa na wengine 17 wamejeruhiwa vibaya baada ya basi walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka katikati yam lima Kitonga wilayani Kilolo mkoani Iringa.

Majeruhi wa ajali hiyo wanaohitaji msaada wa haraka kati ni Vedastus Benjamin (11) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Minazini, Kurasini Shimo la Udongo jijini Dar es Salaam.

Mwanafunzi huyo alikuwa akisafiri pekee yake kutoka Lusaka Zambia kumsalimia baba yake mdogo amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Iringa na kuomba wasamalia wema wafikishe taarifa hizo kwa baba yake mzazi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa, Peter Kakamba alisema ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Isuzu yenye namba za usajili T 218 ACH mali ya kampuni ya Mwashi Express ya Dar es Salaam ilitokea juzi jumatatu majira ya saa 11:30 jioni.

Alisema basi hilo likitokea Tunduma kuelekea Dar es Salaam liliacha njia na kugonga mgema kasha kupinduka na kusababisha vifo vya abiria watutu na majeruhi 17.

Kakamba aliwataja waliokufa kuwa ni pamoja na Clara Dili (32) ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa Lusaka Zambia, Abed Nelson (32) mkazi wa Dar es Salaam na Danny Kawin (43) mfanyabiashara na mkazi wa Zambia.

Alisema dereva wa basi hilo, Benjamin Enock ambaye pia amelazwa katika hospitali hiyo yuko chini ya ulinzi wa jeshi la polisi akisubiriwa apate nafuu ili ahojiwe kwa kuwa uchunguzi wa awali unaonesha ajali hiyo ilitokana na uzembe wake binafsi uliomfnya ashindwe kuchukua tahadhari.

Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Gerlad Guninita alifakia jana katika hospitali ya Mkoa wa Iringa kuwafariji majeraha hayo.

Pamoja na kutoa pole, Guninita alitoa msaada wa fedha na vifaa vya tiba kwa majeruhi waliokutwa hawana ndugu wa kuwasaidia.

Hata hivyo alisema ajali ambazo nyingi zinazuilika zimekuwa zikiongezea mzigo serikali na kuwataka madereva kuwa makini wawapo barabarani.

Source: bongoleaks

No comments:

Post a Comment