masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Tuesday, July 3, 2012

Waandhishi wa habari wa Mkoa wa Iringa wazidi kukumbwa na vitisho > Ofisi ya Mkuu wa Mkoa yatumia mabavu > Waandishi wapangiwa habari za kuandika >IPC yatoa msimamo

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Christine Ishengoma aliyesimama na Kisemeo akisoma katika kitabu


Kitendo cha wanafunzi wa shule za msingi (skauti) kusimamishwa barabarani na kunyeshewa mvua kubwa kwa muda mrefu wakionesha msafara wa makamu wa Rais katika barabara ya Iwawa Wilayani Makete ni miongoni kwa tukio lililosababisha waandishi wa habari katika mkoa wa Iringa kutishiwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Mbali na kunyeshewa mvua, baadhi ya wanafunzi hao waliofika Ikulu ya Makete waliendelea kuambiwa wasimame kwenye mvua wakati wajumbe wengine katika msafara huo wakipata chakula.

Shutuma na lawama zinazoelekezwa kwa waandishi wa habari nchini zinasababishwa na viongozi wengi, baadhi ya wamiliki wa vyombo vya habari na baadhi ya wadau wa habari kutotaka waandishi kuandika mambo yanayowagusa moja kwa moja.

Kazi ya waandishi wa habari ni taaluma kama zilivyo taaluma zingine ambazo hupewa kipaumbele katika bajeti na mambo mengine kimatumizi na kiwajibikaji japo kuwa mara nyingi katika sehemu tofauti waandishi wamekuwa wakinyanyaswa na kutishiwa.

Taaluma hii imekuwa ikiingiliwa mara nyingi na baadhi ya viongozi wa serikali hasa wakurugenzi wa halmashauri mbalimbali, ofisi za mikoa na viongozi wa kisiasa ambao hupenda vyombo vya habari vitumike kwa maslahi yao binafsi.

Baadhi ya ofisi za serikali zimekuwa na mahusiano duni na baadhi ya vyombo vya habari au baadhi ya waandishi ambao hawataki kuingiliwa katika kazi zao au hawataki kufundishwa kazi na kusimamia maadili yao ya kazi.

Wapo baadhi ya viongozi wa serikali ambao wanawapangia waandishi wa habari, babari za kuandika kwa ajili ya kuwalinda wao na kupotosha ukweli kwa jamii. Kwa lugha nyingine naweza kusema wanabadilisha uongo kuwa ukweli kwa faida yao binafsi.

Machi 6, 2012 waandishi wa habari wa Mkoa wa Iringa waliandamana kupinga tabia hiyo inayofanywa na baadhi ya viongozi kuingilia uhuru wa mwandishi na kuchaguliwa habari za kuandika maandamano hayo ambayo yamepokelewa kwa hisia tofauti kwa baadhi ya viongozi wa serikali ambao hawataki kuambiwa ukweli. Viongozi hao wamejitahidi sana kupotoshwa dhamila ya maandamano hayo ya wanahabari.

Maandamano hayo yalitokana na mahusiano mabaya kati ya ofisi ya mkoa na taasisi zake kuwadharau baadhi ya wanahabari wanaofanya kazi katika mkoa wa Iringa.

Moja ya malalamiko ya wanahabari mkoani humo ni ubaguzi na dharau vinavyofanywa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa pamoja na taasisi zake. Kumekuwa na tabia ya ofisi ya mkoa kuchagua chombo cha habari kimoja na kukitumia kama kuitangaza ofisi katika mazuri huku vyombo vingine vikipigwa marufuku kutumika katika ofisi hiyo kwa hofu ya kuwa vinafichua maovu na madudu yanayofanyika na baadhi ya watumishi katika ofisi hizo.

Katika ziara za Naibu Waziri wa Tamisemi Aggrey Mwanri zilizofanyika katika halmashauri zote za Mkoa wa Iringa ofisi ya Mkuu wa Mkoa iliamrisha chombo kimoja tu cha habari huku vingine vikipigwa marufuku japokuwa waziri huyo hakupendezwa na utaratibu uliokuwa umepangwa na ofisi hiyo juu ya matumizi ya vyombo vya habari.

Jambo la kujiuliza ni kwamba, ofisi ya Mkuu wa Mkoa ilikuwa na sababu gani ya kufanya ubaguzi huo wakati vyombo vyote vya habari vinalipa kodi na mapato mengine serikalini na kufanyiwa ubaguzi?

Katika vikao mbalimbali vilivyokuwa vikifanyika kati ya Mkuu wa Mkoa huo Christine Ishengoma na waandishi wa habari amekuwa akitoa kauli za kushirikiana na waandishi lakini kiutekelezaji imekuwa tofauti.

Afisa habari katika ofisi ya Mkuu wa mkoa amekuwa akitumia lugha za kejeli kwa wanahabari wanaohoji kuhusu ubaguzi na mara kwa mara amekuwa akitaka kuwagonganisha vionozi wa Iringa Press Club (IPC) na wanahabari kwa kudanganya mialiko mbalimbali inayotolewa na ofisi hiyo.

Katika ziara ya Makamu wa Rais iliyofanyika mkoani hapa mwezi Februali mwaka huu, afisa habari huyo alilazimika kumrushia mzigo Mwenyekiti wa IPC baaada ya mwanahabari Oliva Motto kuhoji kwa nini ofisi hiyo huwa na ubauzi wa vyombo vya habari katika shughuli mbalimbali zinazohitaji huduma ya habari. Mzigo huo ulilenga kugombanisha mwenyekiti wa IPC na mwanahabari huyo kwa makusudi.

Lalamiko lingine la wanahabari dhidi ya ofisi hiyo ni unyanyasaji. Kumekuwa na kawaida ya wanahabari kutelekezwa wakati wakitekeleza majukumu yanayohusisha ofisi hiyo. Hata hivyo, kuna ziara zingine ambazo mialiko yake ni ya kinafiki. Nasema ni unafiki kwa sababu mtu mzima mwenye akili hutambua kitu ambacho si sahihi.

Katika Ziara ya Waziri Mkuu iliyofanyika Idodi, waandishi wa habari walialikwa lakini hawakupewa usafiri hali iliyosababisha wanahabari hao kuhangaika namna ya kufika mjini.

Katika sherehe iliyofanyika katika kijiji cha Ifwagi Wilaya ya Mufindi ambapo Mkuu wa Mkoa huo alikuwa mjumbe wa siasa, wanahabari walioalikwa walipangiwa nyumba ya kulala wageni ambayo kwa mujibu wa wenyeji wa Mafinga ni maarufu kwa danguro.

Wanahabari hao walilazimishwa kulala katika nyumba hiyo kwa madai kwamba hakuna nyumba nyingine ya kulala wageni yenye nafasi lakini baada ya kugoma walitafuta na kupata nyumba yenye hadhi.

Katika ziara ya Rais aliyoifanya mwishoni mwa mwaka jana huko Ludewa na Njombe, wanahabari walijikuta wakiwa nje ya uzio wa Ikulu ndogo mpaka saa tano wakiwa wametelekezwa bila kujua nini kinafanyika juu yao mahali pa kulala.

Wakiwa katika mazinira ambayo yangewafanya walale nje ya ikulu hiyo, msamalia mwema (Padri wa Jimbo Katoliki la Njombe) akajitokeza na kuwapeleka katika moja ya nyumba za kulala wageni ya Nazareth ambayo humilikiwa na jimbo hilo.

“Kwa kuzingatia utu, ni jambo la kushangaza watu nyumbani kwako kwa ajili ya kushiriki sherehe fulani uliyoindaa mwenyewe, lakini ukawaambia waje na vinywaji na chakula wanachopendelea, shuka na magodoro watakayotumia kulalia kwa sababu sherehe yako ina bajeti ya kuhudumia kundi fulani tu la waalikwa” alisema Padri huyo.

Kwa muda mrefu kumekuwepo na tabia ya baadhi ya maafisa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo Christine Ishengoma kuwatisha wanahabari pindi wanapoandika habari zisizowafurahisha. Vitisho hivi vimekwenda sambamba na kuwalazimisha wanahabari kuandika habari zenye mtizamo fulani kwa manufaa yao binafsi.

Matukio ya wanahabari kutishiwa ni mengi lakini nitalizungumzia moja la hivi karibuni ambalo katika ziara ya Makamu wa Rais aliyofanya wilayani Makete mbali na wanahabari kukubali kushiriki katika mazingira magumu yaliyotokana na masharti magumu yaliyotolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa huo, wanahabari walizuiwa na kutishwa wasiandike habari inayohusu ubovu wa barabara za wilaya hiyo na wanafunzi wa shule ya msingi waliokuwa wamesimama barabara ya Iwawa kama skauti wakionesha msafara njia ya kupita huku wakinyeshewa na mvua kubwa kwa muda mrefu.

Mbali na kunyeshewa mvua, baadhi ya wanafunzi hao waliofika Ikulu ya Makete waliendelea kuambiwa wasimame kwenye mvua wakati wajumbe wengine katika msafara huo wakipata chakula.

Idadi ya wanahabari waliotishwa kwa kuandikiwa barua kwa sababu ya kuandika habari ambazo haziwafurahishi maafisa wa ofisi ya mkoa ni kubwa na baadhi ya wanahari wengine kuvunjiwa vifaa vyao vya kazi.

Pamoja na matutio yote hayo, ofisi ya Mkuu wa Mkoa imeendelea kukaa kimya, haijawahi kutoa tamko lolote lile la kulaani au kukemea. Ukimya huu onaonesha jinsi ushirikiano wa dhati katika kuhakikisha wanahabari wanaendelea kunyanyasika wanapowajibika.

Baada ya waandishi wa habari kuandamana kulaani unyanyaswaji huo, baadhi ya maofisa wamepotosha malengo na mtizamo wa maandamano hayo wakikwepa kubeba lawama hizo kwa kile walichosema wanahabari wameandamana wakidai posho.

Posho siyo miongoni mwa madai yanayolalamikiwa na wanahabari lakini katika mazingira yanayohitaji utu na kufanikisha kazi, siyo busara kuwatelekeza wanahabari pale wanapowajibika kwa manufaa ya jamii.

No comments:

Post a Comment