| George Tito mwanafunzi wa Chuo Kikuu kishiriki cha Mkwawa anayehitimu kitivo cha elimu mwaka huu. |
Wananchi nchini wametakiwa kutowalea viongozi wanaowahadaa kwa kujinufaisha wenyewe na kuwaacha wakiteseka kwa ugumu wa maisha.
Haya yamezungumzwa na George Tito mwanafunzi anayehitimu kitivo cha elimu katika Chuo Kikuu kishiriki cha Mkwawa katika mahojiano maalumu na mtandao huu wa gustavchahe.blogspot.com
Amesema licha ya kuwa bajeti imepitishwa ikiwa na mapungufu, kilichobaki ni kwa wananchi kuchukua uamzi wa kufanya mabadiliko ya serikali ili kuikumbusha serikali iliyopo madarakani kuwa makini pale inapotakiwa kuwajibika.
“Sijafurahishwa na uamuzi wa serikali yetu iliyopo madarakani kwa sababu miaka 50 ya uhuru imekuwa ni janga la ugumu wa maisha na matatozo kwa wananchi badala ya kuwaboreshea na kuwapa uahueni wa kuishi” alisema Tito.
Tito amesema kuwa njia pekee ya kufanya mabadiliko ni kupitia kura pale unapofanyika uchaguzi kwa kuwakataa viongozi wa serikali tawala na kuwaweka wengine.
“Nawaomba wananchi watambue kuwa, kushindwa kwa serikali kutoa ufumbuzi juu ya ugumu wa maisha ni kuwahatarishia zaidi wananchi maisha yao hususani kwa watoto wetu wanaozaliwa leo, kesho na kuendelea. Hivyo, cha kufanya wakati wa uchaguzi ni kuwakataa vionozi hawa na kuwaingiza wengine ili wao wajifunze kupitia wengine” alisema.
Pamoja na kusema hayo, amemtaka Mbunge wa Jimbo la Busega– Mwanza (CCM) kukaa chonjo kwa kuachia jimbo hilo kwa kuwa ameshindwa kuwatetea wananchi wake na kuwatengenezea maisha magumu kila kunapokucha.
“Namtumia salamu Mbunge wa jimbo la Busega huko Mwanza kuwa ajiandae kuachia jimbo kwa kuwa mimi mwenye jimbo narudi baada ya kuhitimu masomo yangu; ameshindwa kuwasaidia wananchi wa jimbo lake na kukubali bajeti mbovu inayowaumiza watanzania” alisema Tito.
Aidha amesema ni jambo la kawaida tu kuwataka wananchi wajiaandae kumkataa Mbunge huyo aliopo madarakani kwa kuwa hana upeo wa kufikiri juu ya kuwasaidia wananchi waliompa kazi.
No comments:
Post a Comment