| Akina mama wakisubiri wabunge katika viwanja vya mkutano Kihesa - Iringa |
| Mh. Zitto Kabwe akiwa na Ole Milia ndani ya kumbi wa VETA Iringa |
| Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi akikabidhiwa cheti cha ushiriki wa upambanaji katika chuo |
| Ole Milia akihutubia wanafunzi katika ukumbi wa VETA |
| Mutaazi Lugaziya mwanasheria akijivua gamba |
| Wananchi wakiwa kwenye mkutano Kihesa |
| Wanafunzi wakicheza ukumbini kusubiri kukabidhiwa vyeti |
| Michael Nguvilaakijivua gamba |
| Mch. Peter Msigwa kushoto, Zitto Kabwe katikakati na Kaimu mwenyekiti Manispaa kulia wakiwa ukumbini |
| Katibu wa UVCCM Singida akijivua gamba |
| Mh. Ziotto akihutubia wananchi Kihesa |
Katibu wa umoja wa vijana CCM Wilaya ya Kilolo Yohana Mvena amejivua wadhifa huo na kuingia katika chama cha Democrasia na Maendeleo CHADEMA katika mkutano ulifanyika jana katika viwanja vya Kihesa Manispaa ya Iringa.
Akijivua wadhifa huo amesema anasikitika amesikitishwa na kitendo cha kuwakandamiza wananchi kwa miaka mingi na kuwafanya kuwa na maisha magu kila kunapokucha bila kuwaonea huruma.
"Nimeamua kujitoa CCM kwa sababu nimekuwa nikiumia kitendo cha kuendelea kuwaumiza watanzania wengangu wakiwemo ndugu zangu huku nikiendelea kutolea taarifa za uongo kuwapa matumaini ya maisha bora wakati ni uongo mtupu" alisema Mvena.
Wakati Mvena akijitoa katika chama hicho, naye katibu wa umoja wa vijana katika Wilaya ya Singida Masifia Hamisi Sumpta ameachia nafasi hiyo na kuingia CHADEMA.
Akikihama chama hicho amesema amegundua kuwa alikuwa anaukumbatia umasikini badala ya maendeleo huku akiwaomba wananchi wamsamehe kwa kuwasababisha umasikini kwa muda wa mika mingi ambayo alikuwa akiikumbati aCCM.
"Kwa miaka mingi nimeukumbatia umasikini wa watanzania badala ya kufanya kazi za maendeleo ya watanzania na taifa kw3a ukumla; najua kuwa mimi ni miongoni mwa wale wote wanaowasababishia umasikini, ninaomba mnisamehe na mnipokee ili niweze kufanya kazi za maendeleo kwa ajili ya umma" alisema na kuongeza kuwa "ukitaka kuwa mjinga, ingia CCM na ukitaka kuwa mnyonyaji na mwizi kupindukia, ingia CCM. Ninawapenda wananchi wenzangu ndiyo maana nimeona hakuna sababu ya kuendelea kukikumbatia chama kisichpo na tija katika maisha ya kila siku".
Michael Nguvila katibu wa baraza lautekelezaji katika Manispaa ya Iringa ni miongoni mwa waliojivua gamba na kuhamia CHADEMA ambaye pia amewataka watawasiendelee kubaki gizani.
"Ninawaomba watanzania tusiendelee kubaki gizani kwa kuwa sasa kumekucha na mwanga unaonekana. Hii ni nchi yetu lazima tuipende, tunakoelekea si kuzuri, kwa yale yote niliyoyaona yakitendeka na CCM kwa muda wote ni unyama mtupu na kama kweli tutaendelea kukikumbatia chama cha mapinduzi, maisha yetu yapo hatarini, kwa kweli kwa muda mrefu nimekuwa nikifanya uchunguzi ni chama gani kitamkomboa mtanzania lakini nimeona CHADEMA ni chama makini kinachopend maendeleo ya watu hakuna kingine" alisema Nguvila.
Wakati hao wakijivua magamba, walisindikizwa na wafuasi wao zaidi ya wanane huku wakisema kuwa nyuma yao wapo watu wengi wanaowafuata ambao wataingia wakati wowote kwa nafasi yao.
Akihutubia katika mkutano huo, Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe amesema bajeti iliyosomwa mwishoni mwa wiki haimlengi mtanzania bali imelenga kuwanufaisha wachache na hivyo kambi ya upinzani imepanga kuisusia.
Amesema umasikini wa watu unasababishwa na mfumuko wa bei za vyakula huku serikali ikishindwa kuthibiti hali hiyo na kuendelea kuwaumiza wananchi.
"Mfumuko wa bei umefikia 18.7% ambazo ni kiwango kikubwa sana kwa maisha ya mtanzania ambapo anatumia 8% kununua chakula iwapo kipato chake kinazidi kushuka siku hadi siku badala ya kupanda kutokana na rasilimali zilizopo. Serikali imeshindwa kurekebisha hali hii na badala yake inazidi kumuumiza mtanzania" alisema Kabwe.
Kwa upande wa mfumko wa bei za vyakula pekee imefikia 25% huku mfumko wa bei ya nishati ukiwa kwenye 28% na deni la taifa likizidi kukua kila siku.
"Tukiachana na mfumko wa bei za jumla, chakula pekee yake imefikia 25%, nishati 28% huku deni la taifa likizidi kukua siku baada ya siku" alisema.
Ikilazimika kila mtu anatakiwa kushiriki kulipa deni hilo, haijalishi mtoto amezailiwa leo au atazaliwa kesho, mzee au mwenye ulemavi kila kichwa kitalazimika kulipa 488,000/=.
"Ili tuweze kulipa deni hilo lote kila kichwa bila kujali mzee, mwenyeulemavu, mtoto au mtoto anazaliwa leo au atazaliwa kesho, kila kichwa kitalazimika kulipa 488,000/=" alisema.
Mwaka jana deni la taida lilikuwa 6 tirioni lakini hadi kufikia mwezi Mei mwaka huu deni limefikia 22 tirioni.
Katika mkutano huo Kabwe aliongozwa Mch. Peter Msigwa Mbunge wa Iringa mjini na kuongozana na Ole Milia na Ali Bananga pamoja na viongo wa Wilaya na matawi iwapo baada ya mkutano huo zaidi ya wanafunzi 90 wanaohitimu katika Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCO) walipewa vyeti vya ushiriki katika hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa VE
Add
No comments:
Post a Comment