| Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mkwawa wakiwa na vyeti vyao vya uanachama nje ya ukumbi wa VIP mara baada ya hafla fupi. |
Vijana wametakiwa kutoa nguvu zao kwa jamii ili kuleta maendeleo na uchumi katika katika taifa kwa kuongeza kipatono.
Haya yamezungumzwa na Charles Ndenga Kaimu Mwenyekiti CHADEMA Manispaa ya Iringa alipokuwa akiwaaga vijana wahitimu katika Chuo Kikuu cha Mkwawa kwenye hafla fupi iliyofanyika VIP Club.
Amesema ili kukabiliana na ukata wa maisha pamoja na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika maisha, vijana hawana budi kuunganisha nguvu zao na kuwa na umoja katika maamuzi na utekelezaji kwa vitendo.
“Nguvu zenu makazifanyie kazi kwa jamii nzima ili kuleta msukumo wa maendeleo ya taifa. Tumieni maamuzi ya pamoja ili mawazo yenu yaweze kujenga hoja” alisema Ndenga.
Amesema ili kutimiza azma hiyo, lazima ujasiri uwepo ili kukakabiliana na changamoto zinazotakiwa kutatuliwa kwa maamuzi magumu.
“Kuweni jasiri katika maamuzi yenu magumu kwani bila hivyo hakuna kitakachofanyika. Msiwe na woga, amueni kisha tenda” alisema.
Amesema katika fursa mbalimbali kunatakiwa wapiganaji halisi wenye kupenda maendeleo bila kutumia ubaguzi, upendeleo au urafiki.
“Fursa mbalimbali zilizopo zinahitaji wapiganaji halisi wenye kupenda maendeleo ya pamoja. Ubinafsi hauwezi kuleta maendeleo. Mkawe wabunge wapiganaji huko muendako” alisema.
Hata hivyo amewataka wawe waalimu bora wa haki za binadamu na kuwafundisha elimu ya uraia ili kila mtu asinyimwe haki zake popote alipo.
“Mkawe waelimishaji wazuri wa wananchi, wafundisheni elimu ya uraia ili waweze kuzijua haki zao popote pale waendapo” alisema.
Jumla ya wanafunzi 53 walipewa vyeti vya uanachama wa chama hicho.
No comments:
Post a Comment