masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Sunday, June 10, 2012

Askofu Mkuu Mtega awakemea wanaochoma nyumba za Ibada: > Asema hayo ni mawazo ya Ibilisi > Ataka kila mtu awe huru kuabudu > Wanasiasa nao wapewa kitimoto

Hivi ndivyo ilivyokuwa katika Kongamano la Ekaristi Takatifu Kitaifa lililoadhimishwa jimboni Iringa. Endelea kufuatilia picha zaidi hapa chini na habari ipo mwishoni





















Mhashamu Baba Askofu Tarcisius J.M. Ngalalekumtwa akitambulisha wageni mara baada ya Misa Takatifu



Wanaozuka na kuchoma nyumba za ibada wametakiwa kuachana na tabia hiyo kwa kuwa hiyo inasababishwa na mawazo ya ibilisi.

Haya yamezungumzwa na Mhashamu Askofu Mkuu Norbert Mtega wa Jimbo Kuu la Songea lipokuwa akihubiri katika Misa ya Maadhimsho ya Ekaristi Takatifu iliyofanyika katika Jimbo la Iringa.

Amesema kukosa maadili kunachangi watu kufanya mambo yao bila kumtegemea Mungu na kuendeleza chuki badala ya kujenga upendo miongoni mwa watu, jamii na jamii, dini na dini, Kanisa na Kanisa, taifa na taifa.

“Kufanya siasa bila kumwabudu Mungu ni uhuni, anayekata tusimwabudu Mungu ni muhuni, kuchoma nyumba za ibada ni ibilisi hata kuzuia wengine wasimwabudu Mungu ni ibilisi na hay yote yanasababishwa na ukosefu wa maadili” alisema Askofu Mkuu Mtega

Amewataka watanzania wawe na akili timamu na iliyokomaa na kupeana uhuru wa kumwabudu Mungu.

“Watanzania tusiingie huko tunakotaka kuingia. Lazime tuwe na akili timamu na zilizokomaa. Kila mtu ana haki ya kumwabudu Mungu na kila mtu ana haki ya kuishi na kila mtu mahala popote na kabila lolote” alisema askofu Mkuu Mtega.

Amesema hakuna dola linaloweza kuzuia kumwabudu Mungu: iwe katiba, kiwe kitabu au serikali hakuna mwenye mamlaka ya kumwabudu Mungu.

“Hakuna dola linaloweza kuzuia kumwabudu Mungu: iwe katika utungaji wa katiba, vitabu au serikali hakuna mwenye mamlaka ya kuzuia kumwabudu Mungu” alisema askofu Mtega.

Amesema maagizo ya Mungu ni kutaka kila Taifa liwe na umoja, kila Kanisa lilipo liwe na umoja na kila serikali iwe na umoja.

“Mungu anatuagiza kila taifa liwe na umoja, kila Kanisa lilipo liwe na umoja na kila serikali iwe naumoja lakini hao wanaozuka na kukataa umoja tusiwaonee haya kwa kuwa wanafuata mawazo ya ibilisi na kuacha maagizo ya Mungu” alisema.

Kwa kila anayemkatalia mwenzake kumwabudu Mungu anamkosea haki na kumnyima uhuru wa maamuzi.

“Anayetukatalia tumwabudu Mungu anatukosea haki. Kutukatalia sisi tusimwabudu Mungu ni kutuchezea” alisema.

Amesema yapo Mambo yanayohusu Mungu ambayo lazima yaheshimiwe bila mzaha.

“Yapo mambo yanayohusu Mungu ambayo lazima yaheshimiwe bila mzahaa. Tuwakemee kwa ushirikiano wale wote wanaoleta chuki na kuchoma nyumba za ibada” alisema.

Katika maadhimisho hayo, juml ya vijana 180 wamepokea Sakramenti ya Ekaristi Takatifu na kuhudhuriwa na maaskofu 19, watawa mbalimbali, viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali, viongozi wa vyama vya kisiasa na viongozi wa serikali.

Kongamano la Ekaristi Takatifu limefanyika Kitaifa jimboni humo ambapo kimataifa linafanyika Dublin Ilerand.

No comments:

Post a Comment