masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Wednesday, July 4, 2012

Afisa mtendaji wa kijiji lawamani

Afisa mtendaji wa kijiji cha Mkalanga Kata ya Ukwega Wilaya ya Kilolo katika mkoa wa Iringa Jeremiah Kasuga analalamikiwa kutumia pesa za kijiji kwa masuala yake binafsi na kutowasomea wanakijiji mapato na matumizi.



Wakizungumza na mtandao huu kijiji hapo wanakijiji wamesema imekuwa ni kawaida kwa afisa mtendaji huyo kutumia pesa za kijiji kwa masuala yake binafsi bila ridhaa ya wananchi au wajumbe wa serikali ya kijiji.


Isaack Nyamoga ni miongoni mwa wanakijiji walioongea na mtandao huu wamesema kuwa mtendaji huyo hashauriki kwa kuwa amekuwa na ubinafsi na kufanya mambo kwa siri bila kuwashirikisha wajumbe wa kamati ya halmashauri ya kijiji.

“Kwa kweli kijiji hiki sasa hatuelewei tunakwenda wapi! Mtendaji wa kijiji hiki anatumia pesa za kijiji kwa masuala yake binafsi, hasomo mapato na matumizi, hashauriki na anapenda kutumia mabavu” alisema Nyamoga.

Amesema kijiji kilijiwekea utaratibu wa kuchanga pesa ili wajenge zahanati ya kijiji lakini hadi leo pesa zilizochangwa hazijulikani zilipo na mpango wa ujenzi haujulikani kama unaendelea au umekufa kutokana na mtendaji huyo kutotoa taarifa za maendeleo ya kijiji.

“Tulijiwekea utarabitibu kuwa, kwa kuwa zahanati vituo vya afya na hospitali ni mbali tuchane pesa ili tujijengee wenyewe zahanati ya kwetu lakini hadi sasa maendeleo hatuyajui na pesa zilizochangwa hazijulikani zilipo na tukitaka kuuliza anatujibu vibaya” alisema.

Mtandao huu umeshuhudia orodha ya wanakijiji 75 waliochanga pesa kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho ikiwa imebandikwa katika ofisi ya kijiji ikionesha kuwa kila mwanakijiji amechanga 10,000/=.

“Idadi ya watu walioorodheshwa hapa ni ndogo ukilinganisha na ile ya wanakijiji ambao hawajaresha michango yao.

Michango ilikuwa inakwenda kwa kasi sana lakini kutokana na mtendaji huyo kutotoa taarifa za maendeleo ya kijiji ikiwemo hii ya michango inayoendelea. Tunapotaka kufanya kazi kwa nguvu zetu zote tunakwamishwa na huyu mtendaji. Sijui tufanye nini!” alisema Nyamoga.

Naye Bi Lazia Mhadisa amesema itafika wakati kila mtu atakuwa anafanya mambo yake bila kujali serikali kwa kuwa wanaotakiwa kuwajibika na kuwahamasisha wananchi kujitoa na kujituma katika kazi za maendelo ya kijiji na taifa wanakuwa na mambo yao binafsi.

“Baba wewe kwa kweli kama kilio hiki kitafika mbele, tunaomba utusaidie sauti zetu zisikike kwa sababu juhudi tunazozitumia ni kwa ajili ya maendeleo ya kijiji chetu zinakwama kwa kukosa uongozi hasa uwajibkaji wa afisa mtendaji.

Tunakuomba utusaidie kusema huko mbele kwa sababu tunawasiwasi kuwa hata pesa zetu tulizochanga zinaweza kupotea hivihivi” alisema Bi Mhadisa.


Amesema ni zaidi ya mwaka hakuna taarifa zozote juu ya maendeleo ya kijiji mtendaji huyo kujiamulia tu kufunua ofisi kwa sababu muda mwini anafanya kazi zake binafsi.

“Ni zaidi ya mwaka mmoja tangu tusomewe taarifa za kijiji chetu. Tulipokuwa tunasomewa taarifa alikuwepo afisa mtendaji mwingine ambaye ameondoka lakini tangu aletwe huyu aliyopo hatujawahi kusika taarifa japo kuwa mwenzake alianzisha jengo la ofissi lile pale na bati zipo ila yeye anashindwa hata kulipaua tu” alisema.

Afisa mtendaji wa kijiji hicho alipofuatwa ofisini ili kutolea ufafanuzi juu ya jambo hilo ifisi ilikuwa imefunwa na alipopigiwa simu alieleza kuwa yupo katika kijiji cha Makungu kikazi.

“Nipo katika kijiji cha Makungu kikazi kwa hiyo ninchoweza kueleza kwa ufupi ni kwamba usiwasikilize wazushi hao kwa kuwa mimi ninafanya kazi na hata hivi sasa nipo kazini huku Makungu” alisema Kasuga.

Alipotakiwa kufafanua anafanya kazi gani huko kijiji kingine alisema nimeshakueleza ujue hilo wala huna haya kujua mimi nafanya nini.

“Mimi nimeshakueleza sasa unataka nini tena? Wewe ujue kama nilivyokueleza hayo mengine unayotaka kujua hayakuhusu” alisema.

Jumla ya shilingi 750,000/= zimechangwa na wanakijiji kwa ajili ya kuanza ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho ambapo Diwani wa Kata hiyo alichangia 50,000/= na kukamilisha kiasi cha shilini 800,000/=.

No comments:

Post a Comment