masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Wednesday, July 4, 2012

Sakata la Dakta Ulimboka wanachuo walonga > Serikali yawakera wasomi > Ukimya wa serikali unaonesha udhaifu wa maamuzi magumu > Wasema ni njama za makusudi


Baraka Mfilinge akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Mkalanga Kata ya Ukwega Wilaya ya Kilolo katika Mkoa wa Iringa

Baraka Mfilinge akiwahutubia wananchi Mkalanga



Mkanyia Timotheo mwanafunzi wa kitivo cha elimu katika Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCO) akiwahutubia wananchi wa kata ya Kitwiru katika Manispaa ya Iringa


Olive Mwakilembe katibu mwenezi CHADEMA tawi la RUCO akiwahutubia wananchi wa Kata ya Kitwiru

Baadhi ya wananchi wa kata ya Kitwiru akiwawasikiliza wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ruaha

Baadhi ya wananchi wa kata ya Kitwiru akiwawasikiliza wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ruaha

Wananchi wa kijiji cha Ipalamwa kata ya Ukwega wakiwa katika majadiliano na katibu mwenezi wa Chadema kabla ya mkutanio uliofanyika katika kijiji cha Mkalanga


Aliyesimama ni katibu mwenezi wa CHADEMA Wilaya ya Kilolo Cosmasi Mmehwa akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Mkalanga

 
Hezlon Lusapi mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Arusha akihutubia wananchi wa kijiji cha Mkalanga kata ya Ukwega

Baraka Mfilinge akimkabidhi Bi. Lazia Mhadisa wa kijiji cha Mkalanga Bendera ya CHADEMA

 
Baraka Mfilinge akimkabidhi mwanchi wa kijiji cha Mkalanga Bendera ya CHADEMA

Kuvamiwa na kupiwa kwa Dakta Stivin Ulimboka kunatokana na ukosefu wa serikali makini isiyojali shida na mahitaji ya watu.

Haya yamesemwa na Baraka Mfilinge alipokuwa akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Mkalanga Kata ya Ukwega Wilaya ya Kilolo katika mkoa wa Iringa.

“Ndugu zangu wananchi, najua mnaweza mkawa mnawalaumu sana madaktari msijue sababu zake ni nini! Napenda kuwaambia kuwa madaktari hawana kosa ila tu mgomo wao unatokana na kutosikilizwa madai yao yanayolenga kuboresha huduma za afya ili hata wewe uweze kunufaika na huduma hizo lakini kwa sababu serikali yetu ni mbovu haina usikivu na haiwajali wananchi inaamua kutumia mabavu badala ya utekelezaji” alisema Mfilinge.

Amewataka wananchi kubadilika na kutambua matatizo yote yanayojitokeza yanasababishwa na serikali mbovu inayokandamiza zaidi wananchi badala ya kuwatengenezea mazingira mazuri ya maisha.

Akitolea mfano katika zao la kahawa ambalo limetelekezwa kwa miaka mingi katika kijiji hicho kwa sababu ya kukosa soko, amesema serikali imeshindwa kuwaboreshea wananchi soko la kahawa huku iking’ang’ania kupandisha kodi ya pombe na sigara.

“Kahawa inaozea porini kutokana na kukosa serikali yenye viongozi makini wenye kufikiri namna ya kuwasaidia wananchi na badala yake wanafikiria pombe na sigara tu katika nchi hii iliyojaa kila aina ya lasirimali; kama viongozi wangekuwa makini, soko la kahawa lingewakomboa wananchi” alisema Mfilinge.

Naye Hezlon Lusapi katika mkutano huo amesema propaganda za serikali zimekuwa ni nyingi kuliko utekelezaji kwa sababu ya ubinafsi uliokithili katika taifa la Tanzania.

Amesema kushindwa kufikiri kwa viongozi kunawapeleka watanzania katika hali ya mateso na kuishi kama wakimbizi ndani ya nchi yao huku wengine wakitumia kodi za nchi kwa ajili ya kujinufaisha wenyewe.

“Vyanzo vya mapato katika nchi hii ni vingi kiasi kwamba kama vingetumika vizuri vingemkomboa mwananchi kwa kiwango kikubwa sana badala ya kushikilia sigara na pombe kama ilivyo katika serikali iliyofilisika kimawazo. Watu wote wakiacha pombe na sigara itakuwaje? Hata mfumko wa bei za bidhaa mbalimbali unatokana na ubovu wa fikra za watu” alisema Lusapi na kuhoji.

Amesma kwa mantiki hiyo migogoro ya wafanyakazi na serikali haitakwisha kamwe kama hakutafanyika mabadiliko ya serikali na vionozi makini na imara wenye kujali shida na maisha ya wananchi wanaolipa kodi kila kukicha.

Mkutano huo ulitanguliwa na mkutano mwingine uliofanyika katika Kata ya Kitwiru ndani ya Manispaa ya Iringa ulifanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA tawi la RUCO na kulaani vikali kitendo alichofanyiwa Dakta Stivin Ulimboka.

Akihutubia katika mkutano huo Mwenyekiti wa tawi hilo Rose Mayemba amesema kitendo hicho hakipendezi hata kidogo na serikali kuendelea kukaa kimya ni kuendeleza unyama katika nchi inayoitwa ya amani.

“Tunalaani vikali unyama aliotendewa Dakta Ulimboka kwa kuwa waliofanya kitendo hicho walidhamilia kumuua kabisa. Hatuwezi kulifumbia macho suala hili kwa kuwa kwa namna moja au nyingine serikali inatakiwa kuwajibika kwa kulijibia suala hilo. Kama huo ndio utatuaji wa matatizo ya madaktari, basi tukubaliane kuwa tumefika pabaya sana” alisema Mayemba.

Amesema jambo la kusikitisha, kuona watu wakiingiza siasa katika sekta muhimu ambazo zinatakiwa kusimamia uhai wa watu.

“Jambo la kusikitisha ni kwamba katika sekta ya afya watu wameingiza siasa na kusababisha nguvu kazi ya taifa kupungua kwa kasi kwa sababu makusudi za watu wachache wenye ubinafsi na kujipenda wenyewe” alisema.

Ameseama kuwa kitendo cha serikali kuendelea kukaa kimya kwa kitendo cha kimyama kilochotokea kwa daktari huyo kinaonesha jinsi kulivyopangwa kwa makusudi.

“Serikali imekaa kimya tangu kutokea kwa kitendo hicho na hapa ndipo panatoa ufafanuzi kuwa hizo zilikuwa ni njama za makusudi” alisema.

Naye Frank Malata amesema kauli ya Mbunge wa Ubungo John Mnyika inazidi kuleta uhai na ufafdanuzi zaidi ikimaanisha kile kilichozungumzwa.

“Watu wengi walimuona Mnyika kama mwendawazimu kule bungeni kwa kauli yake iliyomsababisha kufukuzwa bungeni lakini kwa mtu mwenye akili ya kufikiri na kuona mbali alikuwa sahihi. Mfano mzuri anali katika tukio hili la kuvamiwa daktari na ukimya wa serikali ya chama cha mapinduzi CCM! Ukimya huu ni udhaifu wenyewe unaozungumzwa” alisema Malata.

Amesema uhuru tulio nao kwa sasa ni wa mdomoni tu lakini kivitendo ni kilio kikubwa.

“Uhuru tulio nao ni wa kiimla lakini si ule unaolenwa. Kama ni ule wanaolenga tusingefikia hapa wengine kutekwa na ma kufanyiwa vitu vichafu kama hivi. Haya yote yanasababishwa na viongozi wabovu na serikali mbovu” alisema.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mivinjeni Frank Nyalusi alisema kuwa matatizo, migogoro na na malumbano katika taifa yanasababishwa na kuruhusu watu wenye fikra ndogo watawale fikra kubwa.

“Haya siyo maaizo bali ndivyo serikali ilivyo. Yote haya yanasababishwa na watu wenye fikra ndogo kutawala rikra kubwa. Ndiyo maana Nape alipokuwa akiongea na wananchi wa mkoa wa Iringa pale Sokoni alitaja matusi badala ya kusema vitu vya maendeleo. Ni wakati wa kubadilika” alisema Nyalusi.

No comments:

Post a Comment