masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Saturday, July 7, 2012

Askofu Ngalalekumtwa awataka watanzania kuenzi utamaduni wao


Mhashamu Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa wa Jimbo Katoliki la Iringa akienzi utamaduni wa kimasai


Watanzania wametakiwa kudumisha utamaduni wao na kutoruhusu tamaduni chafu kuharibu utaratibu katika jamii za taifa na Afrika kwa ujumla.

Haya yamezungumzwa Mhashamu Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa wa Jimbo Katoliki la Iringa katika mazunumzo na mtandao huu.

“Utamaduni wetu wa Tanzania ni mzuri na wa kuigwa na watu wamataifa. Tusikubali tamaduni chafu zinazotuharibia taratibu zetu katika jamii kuingia katika maadili yetu” alisema.

Amesema suala la kutunza maadili ni la kila mmoja hapa nchi na katika Afrika nzima na kwa ushirikiano waafrika watapiga hatu mbele kimaadili.

“Afrika kwa ujumla tukishirikiana katika kutunza maadili tutapiga hatua mbele na watu wa mataifa watatuonea wivu lakini tusipokuwa na msimamo sisi wenyewe tutajiharibu na kujichanganya na kupoteza mwelekeo.

Amesema kuwepo kwa utofauti kati ya mwafrika na watu wa magharibi kutawafanya waafrika kuheshimika na kugopwa kwa kuwa mfano wa kuigwa katika nidhamu na heshima mbele za wengine.

“Tukisimamia maadili yetu, watu wa maharibi watatuheshimu wala hawatatulazimisha kufanya mambo ya upuuzi kwa kuwa watatuona ni watu wenye msimamo lakini tukikubali watuamlie nini cha kufanya hata maadili hawatakuheshimu kabisa” alisema.

No comments:

Post a Comment