 |
| Kushoto ni mwakilishi wa Afisa elimu wa Mkoa wa Iringa Dafroza Ndalichako, katika katikati ni Mkurugenzi wa Global Outreach Tanzania Mwalimu Sixtus Kanyama akitoa maelezo mara baada ya wageni kuingia katika maktaba hiyo na kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule ya Lugalo Benjamini Kabungo |
 |
| Wageni waalikwa wakisikiliza maeezo juu ya umuhimu wa maktaba ya kidigitali |
 |
| Farida Ally akigugo kupitia internet |
 |
| Mwanafunzi Farida Ally akiwaelekeza wageni waalikwa jinsi ya kutafuta material kupitia mtandao |
 |
| Kulia ni mwanafunzi wa kidato cha nne katika sekondari ya Lugalo Farida Ally akieleza kile alichokitafuta katika kompyuta kupitia mtandao |
 |
| Baadhi ya wanafunzi waliofika katika uzinduzi wa maktaba ya kidigitali wakisubiri utaratibu |
 |
| Wanafunzi wa shule mbalimbali wakiwa katika makta kusubiri utaratibu kuona jinsi wanavyoweza kunufaika na maktaba ya kidigitali |
 |
| Baadhi ya waalimu wa shule mbalimbali wakiwa katika maktaba hiyo kuona ni namna gani wanafunzi wao wanaweza kunufaika na teknologia bila mwalimu |
 |
| Wageni wakiwa maktaba wakielekezwa namna wenye ulemavu wa kusikia na kuona wanavyoweza kupata elimu kupitia mtandao |
 |
| Mwalimu Charles Kifwe akitoa maelekezo namna ya kutumia maktaba hiyo |
 |
| Mwanafunzi akiwaelekeza wageni waalikwa waliofika katika makta hiyo namna anavyofaidiaka na teknolojia mpya |
 |
| Mkufunzi akionekana katika kompyuta akifundisha sayansi katika maktaba hiyo |
 |
| Wakufunzi mbalimbali wakionekana katika kompyuta za maktaba ya kidigitali wakifundisha |
 |
| Wanafunzi wakionesha namna ya kutafuta matirio kupitia mtandao |
 |
| Mwanafunzi akigugo kupitia maktaba ya kidigitali |
 |
| Wanafunzi wakiwa maktaba ya kidigitali |
 |
| Wanafunzi wakitumia kompyuta katika masomo |
 |
| Mbele ni meneja wa Global Outreach Miraji akicheza na wanafunzi uwanjani |
 |
| Wanafunzi wakicheza wakati wakimsubiri mgeni rasmi aiingie jukuani |
 |
| Mwenye kisemeo ni Mkurugenzi wa Global Outreach Tanzania Mwalimu Sixtus Kanyama akiwakaribisha wageni katika uzinduzi wa maktaba ya kidigitali |
 |
| Wanafunzi wakiwa uwanjani wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi |
 |
| Aliyesimama ni Dafroza Ndalichako mwakilishi wa Afisa Elimu Mkoa wa Iringa akisoma hotuba |
 |
| Mwalimu wa shule ya sekondari ya wasichana Iringa akipokea zawadi za wanafunzi wake |
 |
| Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya Lugalo Benjamin Kabungo akipokea laptop ya mwanafunzi wake. |
Watanzania wametakiwa kujenga utamaduni wa kujiongezea elimu kupitia mitandao mbalimbali ili kupata ujuzi kutoka kwa wataalamu mbalimbali duniani.
Haya yamesemwa na mwakilishi wa Afisa elimu wa Mkoa wa Iringa Dafroza Ndalichako katika uzinduzi wa maktaba ya kidijitali iliyobuniwa na Global Outreach Tanzania yenye makao yake makuu mkoani Iringa.
Ndalichako amesema dunia ya leo ni ya sayansi na teknolojia hivyo ni fursa ya kila mmoja kutumia teknohama katika kujitafutia elimu na utafiti mbalimbali kutoka kwa watu mbalimbali duniani.
“Dunia ya leo ni ya sayansi na teknolojia, hivyo hilia mtu ana nafasi kubwa katika kutumia teknolojia hii ili kujipatia ujuzi zaidi hasa kielimu na utafiti mbalimbali kwa kusaidiwa na watu mbalimbali duniani” alisema Ndalichako.
Mathumi ya maktaba hiyo ni kuwasaidia hata wenye ulemavu wa kusikia na kutoona kupata masomo kwa njia ya mtandao sawa na wengine.
“Ushauri wangu kwa wazazi ni kuwa wawalete watoto wao wafaidi teknolojia hii, hasa wasiosikia (visziwi) na wasio na uoni ili waweze kupata elimu sawa na wengine hata bila kumtegemea mwalimu darasani”.
Amesema itakuwa ni jambo la kushangaza kama watakaofaidika na huduma hizi ni watu kutoka mbali zaidi ya Iringa wakati wenyeji wenyewe hawachangamkii fursa hiyo.
“Pia Shirika limetiliana sahihi na Wizara ya Sayansi ili kusaidia kueneza elimu ya TEHAMA Shuleni katika mikoa ya Kanda nyanda za juu kusini na kanda ya nyanda za juu. Watu waliombali wataifaidi huduma hii kabla yetu tusipo changamka” alisema.
Awali Mkurugenzi wa Global Outreach Sixtus Kanyama alisema maktaba hiyo ni kwa manufaa ya mtu yeyote mwenye nia ya kujifunza kupitia mtandao.
Mwanachama wa maktaba hiyo anatakiwa kulipa ada kiasi cha shilingi 5,000 kwa mwaka iwapo shule wanachama huwa na utaratibu wake kulingana na ratiba za vipindi vya shule hizo.
Global Outreach imeanzisha teknolojia hii ili kuifanya TEHAMA kuwa sehemu ya chombo muhimu katika ufundishaji na kujifunza mambo mbalimbali.
“Ni wajibu wa wakazi wa Iringa Kuitumia nafasi hii adimu ambayo watu wengine wangependa kuipata” alisema.
Katika uzinduzi huo wanafunzi 11 wamepata zawadi mbalimba ambapo mshindi wa kwanza katika kutumia maktaba hiyo amepewa Laptop mpya kwa ajili ya matumizi yake ya nyumbani.
Global Outreach ilianzishwa na kumilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Iringa mwaka 1998. Ilianza na shule moja sekondari ya Pomerini na hadi sasa ina shule 11 katika Wilaya za Kilolo, Iringa, Mufindi na Iringa Manispaa ambapo hadi sasa maktba ina kompyuta 40 zinazotumika na wanafunzi katika kujisomea.
Shirika hili limefanikiwa sana katika kuifanya TEHAMA kusaidia kuinua kiwango cha elimu mkoani kwa mfano kuweka kopyuta kwenye shule 11 za sekondari na kuziwekea umeme wa jua shule mbili za vijinjini.
Shirika hili limefanikiwa sana katika kuifanya TEHAMA kusaidia kuinua kiwango cha elimu mkoani kwa mfano kuweka kopyuta kwenye shule 11 za sekondari na kuziwekea umeme wa jua shule mbili za vijinjini.
Pia Shirika limetiliana saini na Wizara ya Sayansi ili kusaidia kueneza elimu ya TEHAMA Shuleni katika mikoa ya Kanda nyanda za juu kusini na kanda ya nyanda za juu.
Kwa kutumia sekta ya elimu Tanzania itaanda watoto kuingia katika ulimwengu mpya wa ushindani wa kibiashara na kiteknolojia.
No comments:
Post a Comment