masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Friday, May 11, 2012

Mkuu wa Mkoa wa Iringa avuruga Uchauzi RUCO


Rais Jakaya Kikwete



Mkuu wa Mkoa wa Iringa Christin Shenoma amevuruga uchaguzi wa viongozi wa serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ruaha RUCO unaotarajiwa kufanyika 16 Mei mwaka huu chuoni hapo.

Akizungumza na mtandao huu chuoni hapo Spika wa bunge la wanafunzi Sinkala Luka ameshangazwa na kitendo cha mkuu wa mkoa kuingilia uchaguzi wa serikali ya wanafunzi badala ya yeye kuwajibika majukumu yake kwa jamii.

“Kwa ujumla tunashangazwa sana na kitendo cha mkuu wa mkoa kuacha majuku yake kwa jamii na kujiingiza katika uchaguzi wa serikali yetu wanafunzi ambayo haiingiliani kabisa na majukumu yake. Ninaweza kusema kuwa huu ni uvunjivu wa taratibu kwa kuwa kamwe sisi wanafunzi hatujawahi kumuingilia yeye katika nafasi yake” alisema Bw. Luka.

Amesema kuwa wameshangazwa kupata taarifa kuwa Mkuu huyo wa mkoa ametoa tamko la kusitisha uchaguzi pamoja na kuwataka viongozi wa tume ya uchauzi walioapishwa kwa ajili ya kusimamia kujiuzulu bila kutoa sababu zinazomfanya kutoa tamko hilo.

“Kwa kawaida kujiuzulu kwa kiongozi yeyote kunakwenda kikatiba na sheria lakini kitendo cha mkuu wa mkoa kuwataka wanatume hao kujiuzulu bila kutoa sababu zozote kunatia shaka juu ya utendaji na uwajibikaji wake kwa jamii. Sisi wanafunzi tuna katiba yetu ambayo inatuongoza lakini sijui huyu mkuu wa mkoa ametoa tamko hilo kama nani hapa chuoni na kama nani katika uchaguzi huu!” alihoji Bw. Luka.

Kwa mujibu wa katiba ya serikali ya wanafunzi chuoni hapo, ofisi ya spika inapewa mamlaka ya kuteua majina ya waombea kutoka kila kitivo kulingana na uhitaji wa majina hayo.

Mtandao huu ulipomtafuta Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya kutoa ufafanuzi juu ya suala hilo, juhudi ziligonga mwamba kwa kile kilichoelezwa na mhusika wa mapokezi kuwa kuwa mkuu huyo hana nafasi ya kuonana na mtu yeyote.

Mkuu huyo kila alipopigiwa simu ya mezani pamoja nay a mkononi hazikupokelewa. Awali kituo kimoja cha redio kilichopo mkoani hapa walipompigia simu asubuhi kwa ili kupata ufafanuzi wa moja kwa moja kupitia redio simu iliita bila kupokelewa.

Kwa upande wake Mbunge wa Iringa mjini Mh. Peter Msigwa amesikitishwa na kitendo cha mkuu wa mkoa huyo kuingilia masuala ya wanafunzi badala ya kufanya kazi alizotumwa kwa jamii.

“Ndugu mwandishi, suala hili ni la kusikitisha sana. Mkuu wa mkoa amefanya kazi za kada za CCM badala ya kazi zake za uwajibikaji kwa jamii. Ni jambo la kushangaza na kusikitisha sana” alisema Mh. Msingwa.

Imeelezwa kuwa ushawishi huo unatoka kwa mfanyabiashara mmoja anayefanya kazi ndani ya Manispaa ya Iringa kwa kutumia pesa zake kwa kuwashawishi wanafunzi kuchagua viongozi kupitia chama cha mapinduzi CCM.

“Kunamfanyabiashara mmoja ambaye nisinependa kumtaja hapa wa hapa Manispa anatumia pesa zake kuwashawishi wanafunzi kuwachagua viongozi wenye itikadi ya CCM na ndiyo maana mkuu wa mkoa anapigia debe hilo” alisema Mh. Msigwa.

Mh. Msigwa ametoa ushauri kwa mfanyabiashara huyo kuwa ni busara angetulia na pesa zake kufanya biashara zake badala ya kuzingiza katika masuala ya yasiyoendana na kazi zake.

“Mimi ninamshauri tu huyo mfanyabiashara aendelee na kazi zake za kibiashara badala ya kujiingiza katika masuala ya siasa kwani kama ni mapinduzi yatakuja tu bila kulazimishana” alisema Mh. Msigwa.

Hata hivyo amemtaka mkuu wa mkoa kujiepusha na aibu zisizo za lazima na badala yake awajibike katika nafasi yake kwa jamii.

“Mimi namshauri mkuu wa mkoa aache kujidhalilisha kwa kuwa yeye ana nafasi yake ambayo anatakiwa kuwajibika kwa jamii. Tuwaache wanafunzi wawajibike kwa nafasi zao, tusiwaanilie. Wao wana miongozo yao. Tujiepushe na aibu za kipuuzi” alisema Mh. Msigwa.

Baadhi ya wanafunzi wamemtaja mfanyabiashara huyo ambaye jina linahifadhiwa wamesema kuwa kila unapofika wakati wa uchaguzi chuoni hapo amekuwa akifanya hivyo hivyo na kumtaka abadilike.

Katika uchaguzi wa viongozi wa serikali ya wanafunzi chuoni hapo uliofanyika mwaka jana, zilikamatwa kura bandia 1000 na kuzuiwa kuingizwa katika chumba cha kuhesabia kura.

 

No comments:

Post a Comment