masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Thursday, May 10, 2012

Maisha Bora kwa kila Mtanzania ni Ndoto

Hii ni nyumba ambayo mtanzania aliyeadhimisha miaka 50 ya Uhuru anaishi    


Msemo au slogan kwa lugha ya kiingereza unaosemwa na chama tawala yaani chama cha Mapinduzi CCM wa "Misha bora kwa kila mtanzania" unazidi kuwa ndoto kwa wananchi wa nchi hii.

 

Msemo huu ulianza kuvuma sana tangu mwaka 2005 wakati wa uchaguzi mkuu wa viongozi wa Taifa (Madiwani, Wabunge na Rais) ambapo ulikuwa kaulimbiu ya chama tawala ulioambatana na Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya.

 

Katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka 2010 usemi huo huo ukaendelea kusikika masikioni mwa watanzania ukiambatana na "Ari zaidi, Kasi zaidi na Nguzu zaidi.

 

Desemba 9, 2011 nchi ya Tanzania iliadhimisha miaka 50 ya Uhuru. Kauli hizo na maadhimisho hayo yalitarajiwa kuwa furaha kwa wananchi kupata maisha bora.

Ndoto na matumaini ya mtanzania yameendelea kuzikwa siku hadi siku kutokana na wimbi la umasikini linalowakabili licha ya kuwa na utajiri mwingi katika nchi.

Hali hii imebaki kuwa sitofahamu katika maisha ya kila siku. Miongoni mwa maisha magumu ya wananchi hao ni kukosa nyumba bora kutokana na mfumuko wa bei mbalimbali katika bidhaa za vyakula na vifaa vya ujenzi.


Nchi ya Tanzania imejaliwa kuwa na fursa nyingi za utajiri lakini hadi leo wananchi wanaishi kama wakimbizi ndani ya nchi yao. Ni nani atamkomboa mwananchi huyu katika wimbi hili la umasikini? Je, dhana ya utawala bora ililenga nini? Nani ananufaika na utawala bora? Maswali haya yanabaki kama kitendawili kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment