masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Sunday, May 27, 2012

Chiku Abwao (CHADEMA) aipasua CCM Kilolo

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Ibofwe Kata ya Ilole wakimsikiliza Mbunge wa viti maalum Chiku Abwao kwenye mkutano


Chiku Abwao akihutubia wananchi katika kijiji cha Ibofwe.










Zaidi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM katika kijiji cha Ibofwe Kata ya Ilole Wilaya ya Kilolo katika Mkoa wa Iringa wamejiunga na chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA katika mkutano uliofanywa na Mbunge wa viti maalum Chiku Abwao (CHADEMA) uliofanyika jana kijijini hapo.

Akitoa elimu ya uraia kwa wananchi kijijini hapo amesema wasikubali kudanganywa na mtu yeyote bali wajue haki zao za msingi kwa ajili ya maendeleo yao na taifa.

Abwao amewataka wananchi hao kuhoji mapato na matumizi ya vijiji vyao na kutokubali kuburuzwa kwa taarifa za uongo zinazotolewa na baadhi ya viongozi kwani ni za unyonyaji.

Akihutubia katika mkutano huo Wabwao amewataka wananchi kutowaficha wenyeulemavu wakati wa sensa ili waweze kuchukuliwa taarifa zao kwa ajili ya kusaidiwa matatiyo zao.

“Msiwafiche wenyeulemavu wakati wa sensa ili nao waweze kujulikana matatizo yao na mahitaji yao ili waweze kusaidiwa. Ukimfichwa mtu kama huyo unakosa kubwa saba hata utakuwa umemkosea mwenyezi Mungu” alisema Abwao.

Amewataka wananchi kutokuogopa kuhesabiwa kwa kuwa ni utaratibu uliowekwa kisheria kwa ajili ya kupata idadi ya wananchi ili bajeti za serikali ziendane na idadi ya watu.

“Msiogope watakapokuja kuwahesabu siku hiyo kwa kuwa ni utaratibu uliowekwa kisheria ili kupata idadi ya watu wote nchini kusudi bajeti ziendane na idadi hiyo” alisema.

Abwao amesema katika kutungaji wa katiba ingependeya kama ingetolewa elimu juu za katiba iliyopo kwanza ili wananchi waijue na kujua mawazo na mapendekezo juu ya Katiba mpya.

“Itakuwa ni vizuri kama ungetumika muda wa kuelimisha juu ya Katiba iliyopo ili wananchi wijue na waweze kutoa mawazo na mapendekezo yao wakati wa ukusanyaji wa maoni ya Katiba mpya. Kama hili halitafanyika, utungaji wa Katiba mpya hautalenga wananchi. Sisi CHADEMA tunajitahidi kupita maeneo mbalimbali mijini na vijijini ili kutoa elimu ya uraia kwa kila mtu” alisema.

Hata hivyo amekemea tabia ya baadhi ya watu wanaotumia majukwaa kwa kufanya uchonganishi wa kisiasa na madhehebu ya kidini kuwa kauli hizo ni za watu waliofilisika kihoja na sera.

“Ndugu zangu, kumekuwa na propaganda nyingi za baadhi ya watu walifilisika kihoja na sera zao kuwa Chadema ni chama cha Wakristo; waogopeni watu hao kwa kuwa wanatuchonganisha sisi wanasiasa na madhehebu ya kidini. Hayo si maneno ya kweli, hao ni wazushi, waongo na wababaishaji, hawajiamini na uongozi wao na pia ni waoga na matendo yao machafu” alisema.

No comments:

Post a Comment