masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Sunday, June 8, 2014

JENGO LA SHULE YA SEKONDARI KIMALA MBIONI KUANGUKA LIKIWA HALIJAKAMILIKA UJENZI

HALI ya jengo la shule ya Sekondari ya Kata ya Kimala Wilaya ya Kilolo katika Mkoa wa Iringa inazidi kuwa tete kutokana na jengo hilo kudaiwa kujengwa chini ya kiwango na kubomoka huku likiwa linaendelea kujengwa.

Hali hii imewalazimu wananchi kuwabana viongozi wa kata hiyo akiwemo diwani na ofisa mtendaji ili waweze kutolea maelezo jambo hilo.

Diwani huyo Mejus Mgeveke (CCM) pamoja na Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo Deus Wambura wamekataa wito wa wananchi wa Kata hiyo waliowataka kufika kwenye Kikao cha Halmashauri ya Vijiji kilichopangwa kufanyikaia katika Kijiji cha Idunda ili kutolea maelezo juu ya ujenzi wa shule ya sekondari ya Kata hiyo unaosuasua na jengo kuendelea kubomoka huku ujenzi ukiwa haujakamilika.

Viongozi hao wamefikia uamuzi huo baada ya wananchi kuzitaka halmashauri za vijiji vyao kukutana na uongozi wa Kata kujadili na kuwarudishia majibu ya kwa nini jengo la shule hiyo kuzidi kubomoka huku ujenzi ukiendelea licha ya wananchi hao kuendelea kutoa michango huku viongozi wakishindwa kuwasomea wananchi mapato na matumizi miaka yote. 
 
Kwa mujibu wa barua hiyo iliyoandikwa 19 Mei 2014 iliwataka viongozi hao kuhudhuria kikao hicho kilichotarajiwa kufanyika 22 Mei 2014 na kwamba baada ya kikao hicho kingefuatwa na mkutano wa hadhara ili kutoa majibu kwa wananchi.

Wito huo ulikuja baada ya wananchi wa Kata hiyo kuwataka viongozi wa vijiji vyao kutoa majibu yakuridhisha kutokana na maendeleo ya ujenzi wa shule huku wakihoji ni kinachokwamisha kuwasome amapato na matumizi ya jenzi huo tangu mwanzo. 
 
Kutokana na wito huo ofisa Mtendaji wa Kata hiyo Deus Wambura aliandika barua kukataa kuitika wito huo huku akieleza kuwa ofisi yake haiwajibiki kusoma mapato na matumizi kama wananchi wanavyodai.

Mtandao huu umefanikiwa kupata nakala ya barua iliyoandikwa na Wambura ofisa mtendaji wa kata Mei 19 mwaka huu siku hiyo hiyo baada ya kupokea barua ya wito iliyokiri kuwa ofisi yake haiwajibiki kutoa taarifa ya mapato na matumizi.

“Sambamba na hilo, ilishaelezwa kwamba siyo wajibu wa ofisi ya kata kuzunguka katika vijiji kusoma mapato na matumizi badala yake yatasomwa kwenye vikao vya W.D.C baada ya hapo vijiji vitaenda kusoma kwa wananchi” imeandikwa kwenye barua hiyo.

Katika hatua nyingine wananchi wametaka ujenzi huo usimame haraka hadi hapo watakapopatiwa taarifa za mapato na matumizi kwa maelezo kuwa ujenzi huo unawaumiza wananchi na kuwatajirisha watu wachache akiwemo diwani wa Kata hiyo.

Jumla ya wajumbe 17 wa kijiji cha Idunda wametia saini wakiwaunga mkono wenzao wa kijiji cha Kimala kutaka ujenzi wa shule hiyo usimame hadi pale yatakapopatikana na majibu ya kuridhisha.

Wananchi wametoa masikitiko yao kuwa diwani huyo pamoja na ofisa mtendaji wa Kata hiyo wmekuwa wakitumia taarifa za uongo kwa wananchi wanapotaka kuhujumu mali za wananchi.

“Cha kushangaza diwani kwa kushirikiana na afisa mtendaji wa Kata wamekuwa wakitutangazia kuwa kuna ndege itapita usiku wa manane kupima ardhi kwa wananchi tusitoke nje kumbe ndio njia wanayoitumia kuiba sementi na vifaa vya ujenzi ili wasionekane. Wakitangaza hivyo mgambop wamekuwa wakitembea usiku kuangalia watu wanaokuw macho ili wakamatwe kwa ajili ya kuwalipisha faini.

“Ni mara ya pili sasa tunadanganywa, mara ya kwanza walisema ndege itapita usiku kupima ardhi na mara ya pili walisema ndege itapita usiku kumwaga hewa chafu na kuwataka wananchi wasitoke nje wasije wakadhurika kumbe ndio wakati wao wakufanya hujuma” vyanzo vyetu vimeeleza.

Wananchi wa kata hiyo wanapanga kuandamana hadi ofisi za Wilaya kupata majibu ya michango yao inakokwenda ili kupata ukweli halisi wa nguvu zao zinakoishia.

Hata hivyo viongozi wa kijiji cha Kimala, Sadrus Lwanzali mwenyekiti wa kijiji na Festo Mtenga ofisa mtendaji wa kijiji wameelezwa kuwa hawana msaada wowote kwa wananchi kutokana na kumezwa na diwana na ofisa mtendaji wa kata.

“Diwani akiwa na mtendaji wa kata wanatumia mabavu kwa sababu hata viongozi wa vijiji hawana sauti yoyote. Viongozi wa vijiji ni kama wamenunuliwa maana tukiwaagiza hawatuletei majibu yakueleweka” vyanzo vyetu vinaeleza.

Mwishoni mwa mwaka jana mtandao huu uliripoti juu ya jengo la shule hiyo linavyobomoka huku likiendelea kujengwa huku wananchi wakilalamika kutosomewa mapato na matumizi tangu mwanzo wa ujenzi.

Hali ya jengo hilo inazidi kuwa mbaya na kusababisha wananchi kugoma kutoa michango yao kwa maelezo kuwa haiwanufaishi n badala yake inamnufaisha diwani na familia yake badala ya kufanyia kazi inayokusudiwa.

Viongozi hao wanahaha kufanya utaratibu wa kuziba nyufa zinazopasuka katika jengo hilo ambazo zinaonesha hatari ya jengo hilo kuanguka wakati wowote kutokana natatizo linalozidi kujitokeza.

Utafiti wa gazeti hili umebaini kuwa mjenzi wa jango la shule hiyo ni mtwasi wa diwani huyo kwa maana ya kuwa wameolea nyumba moja jambo lililochangia kupeana tenda kirafiki ili diwani huyo awe na maamuzi yake kirahisi.

Awali waliziba nyufa zilizokuwa zimepasuka lakini kutokana na kile kinachodaiwa jengi kujengwa chini ya kiwango, jengo hilo linazidi kudhoofika siku hadi siku.

No comments:

Post a Comment