Mahakama nchini Sudan imemhukumu kifo mwanamke mmoja anayedaiwa kubadili dini yake na kuolewa na mwanamume mkristo.
Mariam Yahya Ibrahim Ishag, ambaye babake ni
muisilamu alishitakiwa kwa kosa la kuasi dini pamoja na kufanya zinaa
kwa kuolewa na mwanamume mkristo , kitu ambacho dini ya kiisilamu
imeharamisha kwa wanawake.
Miriam mwenye umri wa miaka 27 pia
ni mjamzito na anatarajiwa kuadhibiwa kwa kuchapwa viboko kwa kushika
mimba kwa njia ya zinaa kabla ya kunyongwa kwa kuasi dini.
Kwa kawaida wanawake waisilamu hawaruhusiwi
kuolewa na wanaume wakristo ingawa wanaume waisilamu wanaruhusiwa kuwaoa
wanawake wakristo.
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu
Amnesty International linasema kuwa Bi Ishag alilelewa kama Mkristo
muorthodoxi kwa sababu babake hakuwepo naye maishani mwake.
'Kesi ya kwanza'
![]() |
| Serikali imesema kuwa Sudan sio nchi ya kwanza kutekeleza sheria za kiisilamu |
Kesi ya Ibrahim ni ya kwanza ya aina yake kusikika nchini Sudan , kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.
Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu,
wamelaani uamuzi huo wa mahakama na kuitaka serikali ya Sudan kuheshimu
haki na uhuru wa watu kuabudu.
Maafisa wa balozi za mataifa ya magharibi pia wamekemea vikali kesi hiyo na kuelezea asiwasi wao kuihusu.
Maafisa hao wamewataka maafisa wa sheria nchini humo kuangalia kesi hiyo upya na kuhakikisha kuwa Mariam anatendewa haki.
Waziri wa mawasiliano amesema kuwa sio Sudan
peke yake ambako sheria za kiisilamu zinafuatwa na ambako sio sawa kwa
mtu kubadili dini yake, hali hiyo pia ipo nchini Saudi Arabia na katika
nchi zingine zinazofuata sheria za kiisilamu.
Serikali ya Rais Omar al-Bashir inakabiliwa na
changamoto nyingi za kiuchumi na kisiasa hasa baada ya kujitenga na
Sudan Kusini ambako mafuta yake yalikuwa yanatoka mwaka 2011.
Chanzo: bbc swahili


No comments:
Post a Comment