masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Friday, May 16, 2014

PROF. LIPUMBA: RAIS KIKWETE NI MSALITI NA MCHOCHEZI NAMBA MOJA

Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) Profesa Iblahim Lipumba

Mbunge wa Iringa mjini Mch. Peter Msigwa akiwahutubia wananchi wa Iringa.


Bamba Juju Mjumbe wa Kamati Kuu Taifa ya NCCR Mageuzi


Maelfu ya wananchi wa Iringa wakiwa mwenye mkutano wa Ukawa jana.




RAIS Jakaya Kikwete ametajwa kuwa ni msaliti namba moja kutokana nakujidai kuunda kamati ya kukusanya maoni ya katiba mpya na badala yake ameikana tume hiyo na kuidhalilisha kwa watanzania.



Aidha Rais Kikwete ametajwa kuwa mchochezi namba moja na ana nia ya kulifanya taifa kutokuwa na umoja, Amani, utulivu kutokana na kauli za uchochezi ambazo anazitoa mwenyewe pamoja na viongozi ndani ya serikali yake bila kuchukuliwa hatua kali.



Kauli hiyo ilitolewa mjini Iringa na Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa katiba ya Wananchi (UKAWA) Profesa Iblahim Lipumba alipokuwa akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Mwembetogwa.



Mkutano huo ambao lengo lao kubwa ni kuhakikisha wanatoa ufafanuzi ni kwa nini umoja huo umesusia kuendelea na vikao vya Bunge Maalum  la Katiba na kutoka nje.



Profesa Lipumba alisema kuwa kitendo cha Rais wa nchi kudai kuwa iwapo serikali tatu zitapita jeshi litachukua nchi ni uchochezi  mkubwa.



Prof Lipumba alisema kuwa imeonekana wazi kuwa Rais Kikwete pamoja na wanachama wa CCM hawakuwa na nia njema ya kutungwa kwa katiba japo Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM kukubali kuunda tume ya kukusanya maoni  huku akijua kuwa tume hiyo inatumia fedha nyingi ya walipa kodi.



Kiongozi huyo alisema kilichowafanya wana Ukawa kutoka nje ya  Bunge Maalum la Katiba ni kutokana na wajumbe wa bunge hilo kuonesha wazi kutokuwa na nia njema ya kuwa na katiba mpya ambayo ni dira ya maendeleo kwa watanzania.



Aidha Profesa Lipumba alisema kuwa alichokifanya rais Kikwete cha kutaka kuwepo kwa Katiba mpya ni kiini macho na kuwalaghai watanzania.


Alisema Rais Kikwete anatakiwa kuwaomba radhi watanzania pamoja na kuiomba radhi tume ya Jaji Warioba kwa kutumia muda wao mwingi kukusanya maoni ya wananchi kwa uaminifu lakini kutokana na ufisadi wa chama cha mapinduzi Kikwete ameamua kuwadhalilisha viongozi hao ambao wana heshima kubwa ndani ya nchi.

Akihutubia katika mkutano huo pia alisema kuwa nia kubwa ya CCM kutaka kukwamisha mchakato wa katiba ni kutokana na hali yao ya ufisadi.



“Ndugu zangu wote mnajua kuwa katiba ni Roho ya nchi na Katiba ikiwa nzuri vitendo vya wizi wa mali ya Umma vitakomeshwa.



“Lakini CCM haitaki kuwepo kwa katiba mpya hivyo wanafanya kila liwezekanalo ili kuendeleza vitendo vyao vya kuhujumu nchi huku wakiendeleza ufisadi ambao umeliingiza taifa katika hali ya umasikini” alisema Prof Lipumba.



Mbali na hilo Profesa Lipumba alisema kuwa kwa sasa nchi inaendeshwa kisanii kwani Rais Kikwete ana tofauti na Vasco Dagama ambaye alikuwa ni mtu ambaye muda wake wote alikuwa akiwaza kutalii katika maeneo mbalimbali.



“Ndugu zangu wana Iringa kwa sasa nchi yetu inaendeshwa na Vasco Dagama wa karne ya 21 kwani muda wake wote anapenda kutalii, anatumia fedha nyingi kwenda nchi za nje na anatumia fedha za walipa kodi jambo ambalo ni hatari kwa taifa masikini kama hili.



“Tumekosa kiongozi shupavu na mwenye fikra za kuona mbali katika utumishi na ndiyo maana amekuwa akiwachekea wale wote ambao wamekuwa wakitajwa kuwa ni mafisadi wakubwa na kuwasababishia watanzania wasijue hata maisha yao yatakuwaje” alisema Profesa Lipumba.



Alisema kutokana na hali hiyo ndiyo maana serikali wamekuwa maharamia kwa kutaka kuteka mchakato wa katiba na kufanya kila njia ili katiba mpya isipatikane.



Mbali na hilo alisema kuwa anashangazwa na Rais Kikwete kutokuwa tayari kuona haki za binadamu zinaingizwa katika katiba mpya na kuwa sheria inayojitegemea na badala yake amekuwa akitaka haki za binadamu kiwe kipengele tu ndani ya katiba.



Kwa upande wake mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) inasikitisha kuona viogozi wa serikali ya CCM wanaendesha siasa uchwala na zenye vitisho.



Wakati huo huo, Shekh Rajab Katimba kutoka katika Shura ya Maimum alisema Rais Kikwete alipoteua tume ya Katiba alikonekana kufanya jambo la maana na la haki lakini cha kushangaza amekuja kuitukana tume aliyoiteua mwenyewe.



Alisema maoni yaliyomo kwenye Katiba si ya Jaji Warioba kama Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na chama chake bali ni maoni ya wananchi ambayo yanatakiwa kuheshimiwa.



Alisema haiwezekani hata siku moja kukawa na amani kama hakuna haki na kwamba CCM haitaki uwazi na kuwatukana waasisi wa Muungano jambo ambalo walianza kuwatukana katika kulivunja Azimio la Arusha.



“Cha kushangaza baada ya wananchi kutoa maoni rais Kikwete ameonesha usanii waziwazi na kuitukana tume ya Katiba pamoja na kuwatukana wananchi ambao wametoa maoni hayo. Ulimwengu tunaokwenda nao si ulimwengu wa kudanganyana bali ni ulimwengu wa uwazi. Tusahau utofauti wetu wa vyama, huu ni wakati wa kutafuta maendeleo ya wananchi.



“Kiongozi yeyote anayesimama na kuchochea eti tukiwa na serikali tatu kutakuwa na udini ni muongo mkubwa tena ni mchochezi wa machafuko. Hiyo ndiyo tabia ya CCM kutuchonganisha sisi wananchi tulioishi kwa kuheshimiana katika imani zetu kwa zaidi ya miaka hamsini” alisema.



Naye Bamba Juju Mjumbe wa Kamati Kuu Taifa ya NCCR Mageuzi alisema CCM wanatapeli wananchi kwa maneno mepesi mepesi kwa hoja zisizo na msingi huku wakishindwa kujenga hoja ya kuwa na Serikali mbili kama wanavyotaka.



Alisema nia ya CCM ni kuendelea kuwatengenezea wananchi umasikini kwa kuendeleza ubabe na ufisadi wao uliokithiri katika chama chao cha kwa kutaka kuendelea kuwaficha wananchi ukweli kuhusu tunu za Taifa.



“Umasikini si kitu kinachokuja kama ajali bali ni kitu kinachotengenezwa. Umasikini tulio nao Watanzania umetengenezwa na CCM. Hoja na misingi ambao CCM wanashindwa uielewa ni umoja wetu.



“Kitu ambacho hatuji ni kwamba, ukishakuwa mtumishi wa serikali hutakiwi kufungua akaunti nje ya nchi lakini hawa wenzetu CCM wanataka waendelee kuwaibia wananchi ili wakafungue akaunti zao nje kama wanavyofanya sasa.



“Tujadiliane kujenga hoja pale bungni lakini siyo kukataa maoni ya wananchi. Ukosefu wa amani na haki havifungamani hata siku moja” alisema.

No comments:

Post a Comment