WANAWAKE wametakiwa
kutotumia utandawazi kama kigezo cha mmomonyoko wa maadili katika jamii nchini.
Haya yamezungumzwa na
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Dkt. Letisia Warioba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa
Iringa Christine Ishengoma katika maadhimisho ya siku ya wanawak duniani
iliyofanyika jana katika viwanja vya Mwembtogwa katika Manispaa ya Iringa.
Amesema wanawake
wanakumbushwa wajibu zao katika jamii ili kulea familia zenye mwenendo mzuri na
kutoruhusu utandawazi kuvuruga maadili hasa tamaduni za kiafrika.
Akisoma hotuba hiyo
Warioba amesema wanawake wasiwaruhusu watoto wao kufanyishwa kazi kwa
kunyanyasika sambamba na kulipwa ujira mdogo.
Ameikumbusha jamii
kushiriki shughuli za haki katika usawa bila kumbagua mwanamke na kuhakikisha
kuwa hakuna unynyasaji wa kijinsia unaofanyika katika familia.
“Kina mama tutoe
maamuzi ya busara pale inapobidi. Wazazi tusibague watoto wetu katika fursa
bila kumbagua mtoto wa kike kama hawezi chochote bali wapeni nafasi sawa”
amesema.
Wakisoma risala mbele
ya mgeni rasmi, wanawake wamesema wanaiomba jamii itambue mchango unaotolewa na
wanawake mahali popote duniani.
Wamesema ndoa ndoa
nyingi zimekuwa zikiathiria na janga la UKIMWI ambalo husababisha vifo kwa
wenza na kuongezeka kwa kazi ya idadi ya wajane au wagane na watoto wanaoishi
katika mazingira hatarishi na yatima.
Hata hivyo wamesema
katika Manispaa ya Iringa wamekuwa wakipeana mbalimbali kwa pupiga vita
kujiingiza katika ngono, kujiepusha na mila na desturi, imani potofu na mazoea
hatarisi kuhusu uhusiano wa unyumba na mambo ya uzazi.
“Elimu juu ya UKIMWI
imetolewa kwa wanandoa na wafanyabiashara kutoka makundi mbalimbali ili
kuwawezesha wanawake ambao ndio wanaahirika zaidi na kubeba mzigo mkubwa kwa
kulea watoto yatima na wagonjwa wa UKIMWI” wamesoma kwenye risala.
Katika kutekeleza kwa
vitendo msemo wa lugha ya Kiswahili usemwao “mtoto wa mwenzaio ni wako”,
kupitia mfuko wa wanawake wa Manispaa ya Iringa wameweza kusaidia familia zenye
kulipa karo ya shule kwa watoto 18 waliochaguliwa kujiunga na shule za
sekondari jumla ya sh. 400,000/= ambapo watoto 98 walipewa mahitaji mbalimbali
kama vile sukari, unga wa sembe, sabuni, madaftari na mafuta ya kupikia ambavyo
vilitokana na michango ya siku ya mwanamke duniani ya mwaka 2013.
Vile vile sh. 500,000/=
zilitolewa kwa ajili ya kugharamia matibabu na huduma mbalimbali ya vipimo
katika hospitali ya Rufaa ya Taifa Mhimbili kwa kijana mwenye mazingira magumu
mwenye tatizo la kibofu cha mkojo anayetoka katika Kata ya Ruaha katika
Manispaa ya Iringa.
Katika ufumbuzi wa
kudumu wa tatizo la familia zenye mazingira magumu, wanawake wamefungua akaunti
ambayo itatumika kuhifadhi fedha ambazo zinatokana na michango ya watu
mbalimbali ambayo hadi sasa ina jumla ya kiasi cha sh. 1,145,500/=.
Wakati wa maadhimisho
hayo watumishi wa ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa walitoa msaada wa chakula
wenye thamani ya Sh. 181,000/= kwa kituo cha watoto yatima cha FARAJA HOUSE
Mgongo kilichopo Kata ya Nduli ambapo vikundi mbalimbali vimetoa zawadi kwa ajili ya kuwasaidia vituo vya watoto yatima.
Maadhimisho ya siku ya
wanawake duniani yalianza kuadhimishwa tangu mwaka 1945 huku Tanzania ikianza
kuadhmisha rasmi mwaka 1995 ambapo siku hii huadhimishwa 8 Machi kila mwaka.
No comments:
Post a Comment