masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Saturday, December 7, 2013

PROFESA MSOLLA ALITUDANGANYA: WANANCHI

Hifadhi ya Udzungwa

WANANCHI wa Kilolo wamemtaka Mbunge wao Prof. Peter Msolla (CCM) kutorudi tena kuomba kura kwao kama hatatekeleza ahadi zake alizowaahidi mwaka 2011 wakati wa kampeni za uchaguzi Mkuu.

Wananchi hao wamesema wamefikia hatua hiyo kutokana na Mbunge huyo kuwahadaa kwa mambo mengi ambayo hajawahi kutekeleza hata moja huku akipotea jimboni kwa muda mrefu baada ya kupata alichokuwa akihitaji.

Wakizungumza na mtandao huu, wakazi wa kijiji cha Udekwa Kata ya Udekwa Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa wamesema hawakutarajia kama kiongozi mwenye hadhi ya uprofesa angeweza kuwadanganya watu.

Wamesema kwa kutumia cheo chake aliahidi mambo mengi ikiwemo barabara, minara ya simu na mambo mengine mengi ambayo hadi sasa hakuna hata moja lililoonekana kufanyika zaidi ya wananchi kunyanyasika.

Katika hatua nyingine wananchi hao wakiongea katika mkutano wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) uliofanyika kijijini hapo juzi, wamesema ikiwa wao ndio wapo jirani na hifadhi ya Udzungwa hawaoni manufaa ya hifadhi hiyo kutokana na kuwa na viongozi wazushi, waongo na vipofu ambao hawaoni umuhimu wa hifadhi hiyo.

“Tulitegemea Mbunge alipoahidi barabara hii kujengwa tutanufaika na hifadhi hii kwa sababu ya kufikiwa kwa urahi na watalii lakini cha kushangaza imekuwa ni rahisi kusafirisha mzigo kutoka mjini kwenda Dar es Salaam kwa bei nafuu kuliko kutoka hapa kijijini kwenda Mjini.

“Utashangaa gunia moja la maharage linasafirishwa kwa shilingi elfu nane hadi elfu kumi kutoka hapa kijijini kwenda Iringa mjini wakati gunia hilo hilo linasafirishwa kwa shilingi elfu tatu kutoka Iringa mjini kwenda Dar es Salaam. Hii inatokana na viongozi wetu kuwa wanafiki na waongo kutufanya sisi watoto” alisema Baraka Mfilinge.

Wananchi wao wamesema itafika mahali ambapo watafanya maandamano hadi halmashauri ya Kilolo kudai barabara kwa kuwa ni haki yao ya msingi ambayo wanahitaji kupata kwa kuwa kodi zao zinatakiwa kuwanufaisha.

Akiongea na wananchi wa Udekwa kwenye mkutano huo, mlezi wa Chadema Wilaya ya Kilolo Brian Kikoti alisema daktari aliyeshindwa kutambua ugonjwa, hawezi kuutibu na kwamba viongozi walioshindwa kutambua matatizo ya wananchi hawawezi kuyatatua.

Amesema licha ya nchi kuwa na sheria, hazifanyi kazi kwa usawa na badala yake zinapendelea upande mmoja kwa maana ya kuegemea katika Chama cha Mapinduzi badala ya kusimamia haki za wananchi.

“Ikiwa diwani anashindwa kuwasemea watu wake, ni sawa na pipa la taka. Ni lazima tutafakari juu ya watoto wetu na akina mama kuwa ni maisha gani tunataka kuishi kwa sasa na kwa baadaye. Sisi wenyewe ndiyo tunaojiingiza mkenge kwa kuchagua viongozi walafi, wanafiki, wababaishaji na waroho.

“Utalii katika hifadhi zetu utachelewa kwa sababu viongozi tulio nao hawana upeo wa maendeleo bali wana upeo wa matumbo yao. Kama wangekuwa na akili ya maendeleo wangeboresha miundombinu katika ili hifadhi zetu ziweze kufikika kirahisi” alisema.

Endapo barabara ya Ilula – Udekwa ingejengwa, ingerahisisha kufikiwa kirahisi hifadhi ya Udzungwa kwa upande wa Udekwa ambapo hata hivyo Mbunge huyo aliahidi kujenga barabara ya Mahenge – Mabondwa (Udekwa) lakini hadi leo haijaguswa.

No comments:

Post a Comment